Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Novemba 22-2026 ndiyo siku Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwaich, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam alitangazo kuundwa kwa Dekania mpya ya Chanika. Tangazo hilo lilitolewa kwenye sikukuu ya kilele cha Mavuno Novemba 22-2026. .Parokia zinazounda Dekania hii ni (8), ambazo ni; Chanika, Zingiziwa , Mvuti, Msongola B ,Chakenge, Nyebulu,Yongwe na Parokia Teule za Kurutini, Homboza na Vikongoro.
Kabla ya hapo parokia hizi zilikuwa sehemu ya Dekania ya Pugu lakini baadaye zilimegwa na kuunda Dekania mpya ya Chanika. Askofu Mkuu alimteua Pd. William Sindano kuwa Dekano mpya wa Dekania ya Mt. Carlos Acutis- Chanika
Parokia za Dekania hii zinapatikana ndania ya wilaya ya Temeke . Asili ya shughuli za wakazi wa maeneo haya, zaidi sana ni biashara ndogo ndogo, na kwa sababu wako ukanda wa pwani maeneo mengi yametawaliwa na kilimo cha mihogo, minazi na kwa sehemu ndogo mikorosho. Baadhi yao ni wafanyakazi katika sekta mbalimbali.
Madekano walioongoza Dekania ya Mt. Carlos Acutis - Chanika tokea kuundwa kwake.
· Padre William Sindano – Dekano --- 2026-----
§ Padre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam
· Padre (Shirika) –
Padre (Shirika)
· Padre (Names)
Padre (Shirika)
Ndani ya Dekania hii, wakazi wa maeneo haya kwa kiasi kikubwa wamechangamana kwa dini na makabila,
Maelezo ya mawasiliano
PD. WILLIUM SINDANO
Mkuu wa Dekania ya Chanika
Phone : 0682 656330