Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Dekania ya Mt. Yosefu inaundwa na Parokia ambazo baadhi yake zina historia ndefu na pia ni kongwe zikiwemo; Kanisa Kuu la Mt. Yesef lenyewe lililozaliwa mwaka (1889), Parokia nyingine ni- Bikira Maria Mama wa Fatima- Msimbazi (1952), Chang’ombe -St. Francis Xavery (1960), Upanga (1968), Kurasini - Mt. Maurus (1970), Mburahati (1974) na Mafia (1997). Parokia zote hizi ni zao Mt. Yosef. Ukiangalia hata majengo ya Makanisa ni ya muda mrefu ukilinganisha na parokia zinazojengwa sasa.
Kwa sasa Dekania ya Mt. Yosefu inaundwa na Parokia zipatazo 14 ambazo ni; Parokia ya Mt. Yosef, Msimbazi, Keko, Upanga, Changombe, Mburahati, Mafia, Muhimbili, Kurasini, Buguruni, Mtoni, Mikoroshoni. pamoja na Parokia Teule za Baleni na Gonge.
Nakushauri fuatilia Parokia moja baada ya nyingine ili ujifunze zaidi.
Madekano waliopata kuongoza Dekania hii ni;
1.Dennis Wigira.
♦Padre wa Jimbo la Dsm.
2.Casmir Kavishe -Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafransisco (OFM
Cap)
4.Padre Efreim Oga
4.Padre Anthony Mashaka Shakijuu
5.Amandus Sunga.- Pd wa Shirika la Ndugu
Wadogo Wafransico (OFM. Cap)
Maelezo ya mawasiliano
Pd. Denis Wigira
Mkuu wa Dekania ya St. Joseph
Phone : 0682 656330