Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Waamini walijifunza kuhusu historia ya msalaba
Katika kuangali historia ya msalaba walipitishwa kuangalia
desturi yake kabla ya Yesu kusulibiwa Msalabani, ambapo watu wengi wanadhani
kuwa msalaba ulianza wakati wa Kristo kumbe sivyo
Inasemekana Msalaba ulitumiwa na mataifa mbalimbali kwa
matumizi tofauti tofauti enzi hizo wengine kama alama kwenye mila na tamaduni
zao, na Wengine walitumia kama Kitu cha kutolea adhabu ya wahalifu wakubwa..
Mwana historia maarufu Dkt. Cilliers anasema kwamba
kusulubiwa ilikuwa pia ni asili ya Waashuri Waajemi na Wababiloni kama desturi
yao, na walisulubishwa kwenye miti badala ya msalaba rasmi.
Inasemekana adhabu ya kutundikwa msalabani ilianzishwa Misri na Syria, baada ya utawala wa Alexander
the Great, Warumi walijifunza mbinu hiyo na "kuikamilisha kwa miaka
500", pia adhabu hiyo ilitekelezwa Israel ya kalena aina hii ya adhabu ilikuwa tayari ikitumiwa
kabla ya Warumi kufika
Mwanahistoria Mroma-Myahudi, mwanasiasa, na mwanajeshi
Flavius Josephus, aliyezaliwa Yerusalemu katika karne ya kwanza BK. Katika
masimulizi yake ya utawala wa Alexander Jannaeus (125BC-76BC), ambaye alitawala
Wayahudi kwa miaka 27, alitaja kusulubiwa kwa wingi karibu 88BC. 2 Lakini
kulingana na Dr Cilliers, Warumi ndio waliojumuisha aina mbalimbali za misalaba
kwa aina hii ya adhabu - ikiwa ni pamoja na umbo la X.
Waamini walipata bahati ya kujifunza aina mbalimbali za
misalaba iliyotumika katika adhabu ikiwemo yenye umbo la X, T
Waamini walifundishwa kuhusu umbo la Msalaba wa Yesu na maana
yake katika Maisha ya wakristo lakini pia walifahamu kuhusu sifa ya Msalaba wa
Kikatoliki na Baadhi ya maumbo ya Misalaba iliyotumika baada ya kristo
kusulibiwa. Walijifunza pia alama muhimu walizopaswa kuzingatia wakati wanapouona
Msalaba nazo
Msalaba kama ishara ya Ukombozi
Asili ya matumizi ya Msalaba ni kama ilivyoonyesha hapo juu,
lakini baada ya Kristo Yesu kusulibiwa kwa kutumia Msalaba, alibadili maana ya
asili ya matumizi yake, kwani kupitia kifo chake juu ya Msalaba tumepata
Ukombozi, hivyo kutokea hapo Msalaba unatizamwa kama chombo kilichotumika
kutuletea Ukombozi. Waefeso,2:11-22, Wagalatia, 3:13-14, Wakolosai, 1:20,
2:14-15
Kwa kadiri ya Mtume Paulo, Baada ya Yesu kufufuka ametuachia
kumbukumbu muhimu ambayo ameielezea
vizuri katika nyaraka zake, 1, Wakorinto, 1:18, Kwa sababu neno la msalaba kwao
wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Mtume Paulo
katika kazi ngumu alizofanya anaona Msalaba wa Kristo ndiyo Fahari yake.
Wagalatia, 6:14,
Waamini walijifunza pia matumizi ya Msalaba, Umuhimu wa kufanya Ishara ya Msalaba na pia njia ya Msalaba katika maisha ya mkristo
. (1, Wakorinto, 1:18,) Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
1. Uelewa kuhusu Msalaba
2. historia ya msalaba
3. Aina za Misalaba
4. Umuhimu wa Msalaba kwa waamini Wakristo
5.namna ya kuutambua msalaba
6. Matumizi ya Msalaba
Ushiriki wa wababa na vujana kwenye semina bado ni mdogo
kutokuwepo kwa semina za mara kwa mara kuhusu msalaba
kupelekwe semina za kutosha
Hakuna kumbukumbu ya somo iliyopatikana...