Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Parokia ya Mt.Teresia wa Avila- Kibwegere ni mojawapo ya Parokia zinazounda Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Neno “kibwegere”asili yake ni makabila ya kusini mwa Tanzania, maana yake Shimo la Kutahiria. Wamakonde, Wamatumbi na Wayao makazi yao yalikuwa Kibamba.Kibwegere ilikuwa pori, hivyo watoto wa kiume walikusanywa wakati wa kutahiriwa (jando) walipelekwa Kibwegere, ndiko waliwekwa.
Uzinduzi wa Kigango cha Kibwegere ulifanyika Mwaka 1996 na kuwekwa chini ya mwombezi Theresia wa mtoto Yesu.ujenzi wa Kanisa kubwa ulianza 1990. Ujenzi wa nyumba ya Mapadre ulianza rasmi tarehe 17/03/2013.
Parokia ya Mt. Theresia wa Avila- Kibwegere ilitangazwa rasmi tarehe 7/7/2014 na Mwadhama Polycarp Kardali Pengo ikiwa parokia ya (94) katika Jimbo la Dar es Salaam. Parokia ilitokana na Kigango kilichoitwa Teresia wa Mtoto yesu. Paroko wa Kwanza ni Pd. Ovadius Elizabeth Paulo Nachenga, Msaidizi alikuwa Pd. Gaspar Matumaini na Baadaye Pd. Romuald Mukandara
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Huduma ya Maombi: Kikundi kinachosaidia waamini kukuza maisha ya maombi na tafakari.
- Kikundi cha Wanawake wa Mtakatifu Theresia: Wanawake wanashirikiana kujifunza na kueneza maadili ya Kikristo kupitia huduma za kijamii.
- Huduma za Vijana: Vijana wanapewa fursa ya kujifunza na kushiriki katika maisha ya kiroho kupitia shughuli mbalimbali.
- Huduma za Familia: Familia zinashirikiana katika mafunzo na ibada za pamoja ili kuimarisha mshikamano wa kifamilia.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...