Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Ukatoliki katika eneo la Misugusugu ulianza na familia tano (5) mwaka 1971 zikiongozwa na Marehemu Mzee Nemes Daudi Luzua aliyehamia katika Kijiji cha Misugusugu kutoka Matombo Morogoro akiungana na familia za Mzee Athanas Masenga, Marehemu Mzee Arbogast Matembele, Amandus Mponda, na Gustav Mtumbuka waliohamia kutokea Kipatimo Kipatimu.
Familia hizi zilikutana kwa Mzee Nemes kwa sala chini ya mti wa mkorosho tangu mwaka 1971. Wakati huo hapakuwepo Kigango wala Jumuiya. Wengi hawakuwa wamebatizwa wala kufunga ndoa. Mwaka 1976 idadi ya waumini iliongezeka kidogo ikabidi kuomba kutumia chumba cha darasa katika Shule ya Msingi Misugusugu kwa ajili ya ibada ya Misa siku za Jumapili.
Mwaka 1980 Misugusugu ilitangazwa kuwa Kigango rasmi chini ya Parokia ya Tumbi/Kibaha. Mwaka 1995 Kigango cha Mlandizi kikawa Parokia, Kigango cha Misugusugu kikawa chini ya Parokia ya mlandizi. Julai 2016 ujenzi wa nyumba ya mapadri ulianza na kukamilika Juni 2017. Mwadhama Polycarp Pengo alitangaza Kigango cha Misugusugu kuwa Parokia ya Mt. Polycarp siku ya tarehe 7 Julai 2017. Ndoa 27 zilibarikiwa
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Huduma ya Liturujia: Inasaidia kuandaa na kuendesha ibada kwa nidhamu na utukufu.
- Kikundi cha Vijana wa Mt. Polycarp: Vijana wanajifunza na kushiriki katika shughuli za kiroho na kijamii.
- Kwaya ya Parokia: Inahamasisha waamini kwa nyimbo zenye ujumbe wa kiroho.
- Huduma za Wanandoa: Husaidia wanandoa kujenga ndoa zenye imani na mshikamano.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...