Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Historia yetu ilianza Mnamo Mwaka 1992 kama kituo cha Sala katika Shule ya Msingi Kijitonyama, wakati huo baadhi yao walikuwa wakisali Parokia ya Mwenge na wengine Parokia ya Mwananyamala.
Ndipo mwishoni mwa Mwaka 1999, lilipatikana eneo mahali lilipo kanisa sasa na ikajengwa Nyumba ya Sala. Mnamo Mwaka 2000 katika mkesha wa Krismasi waamini walihamia rasmi na kuendelea kusali kama kituo cha Sala hadi mpaka 2002 tulipopandishwa hadhi na kuwa Kigango cha Kijitonyama chini ya Parokia ya Mwananyamala .
Baada ya uzinduzi wa
nyumba ya Mapadri mwaka 2015, Kigango cha Kijitonyama kilipatiwa Padri. Tarehe 06/01/2016 Siku ya Epifania, Kigango
cha Kijitonyama kilitangazwa rasmi kuwa Parokia Teule. Tarehe 26/04/2016 Kigango kilitangazwa kuwa Parokia Teule Mt. Yakobo Mkuu
Mtume. Padri Arnold Babu Tarimo aliteuliwa kuwa paroko.
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Kwaya ya Parokia: Kwaya ya Kijitonyama inahusika na uimbaji wa nyimbo za ibada, zinazosaidia waamini kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.
- Huduma ya Familia: Huduma hii inajitahidi kuimarisha familia na ndoa kwa kuzingatia maadili ya Kikristo.
- Kikundi cha Vijana: Vijana wanahamasika kutumikia jamii na kushiriki katika ibada za parokia.
- Huduma ya Jamii: Huduma hii inatoa msaada kwa wahitaji, ikiwa ni pamoja na misaada ya chakula na kifedha.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...