Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Historia ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu – Buza inaanzia mwishoni mwa miaka ya 1960. Waamini wa kwanza Buza walikuwa wanasali parokia ya Yombo Kiwalani, kutokana na umbali waamini walikubaliana kusali Buza. Walianza kusali chini ya mwembe. Baadaye walipata pesa na kununua kiwanja toka kwa Bw. Kigola mwaka 1970 hapo ndipo walipoanza kujenga Kanisa dogo la miti, walikalia magogo ya nazi.
Mwaka 1985 waliongeza eneo. Kanisa la kudumu lilinza kujengwa mwaka 1998. Msimamizi wa ujenzi alikuwa Fr. Luis. Kanisa lilipo kamilika yalitengenezwa mabenchi ya kudumu mwaka 1999. Baada yah apo kKanisa lilizinduliwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo 22/10/1999.
Kardinali Pengo aliwafahamisha waamini wa buza ya kuwa, ili waweze kuwa Parokia sharti wajenge nyumba ya Mapadre Kwanza. 2003 ujenzi ulianza msimamizi akiwa Pd. Camili, na kufikia 2005 nyumba ilikamilika na Tar 02/10/2005, Mhashamu Methodius Kilaini Askofu Msaididi wa jimbo la Dar es Salaam alizindua. Buza ilitangazwa parokia Tar 22/11/2011 na Kutabarukiwa 2015 na Mwadhama Polycarp K. Pengo. PAroko wa kwanza alikuwa Pd. John Waldrep
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Kwaya ya Mt. Theresia: Inaburudisha na kugusa roho za waamini kwa nyimbo zenye ujumbe wa kiroho.
- Huduma ya Familia: Inatoa msaada wa kiroho na kijamii kwa familia zenye changamoto, huku ikihamasisha mshikamano wa kifamilia.
- Huduma ya Vijana: Vijana wanashiriki shughuli mbalimbali za kiroho na kijamii, wakihamasishwa kuwa viongozi wa kesho.
- Huduma ya Upendo: Wanajumuiya wanajitolea kusaidia jamii, hasa wale walio katika mazingira magumu.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...