KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Parokia
Parokia ya Kitunda

Parokia ya Roho Mtakatifu Kitunda ilitangazwa rasmi kuwa Parokia tar 07 Julai 2010 na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika sherehe za Upadrisho zilizofanyika Parokia ya kristo Mfalme Tabata Dar es Salaam, kabla ya hapo Parokia ya Kitunda ilikuwa moja ya Vigango vinne vya Parokia ya Mt. Agustino Ukonga, Vigango hivi ni Magole, Mwanagati, na  Mt. Monika Mizizini ambazo zote kwa sasa ni pParokia kamili. Parokia ya Roho Mtakatifu Kitunda ipo Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es salaam, kilometa 4 kutoka Banana Jirani na uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Kwa upande wa mashariki inapakana na Parokia za Mwanagati na Buza, upande wa Kusini Parokia ya Kivule na Upande wa Magharibi Prokia ya Ukonga

Kitunda ni moja ya Parokia zinazounda Dekania ya Ukonga zikiwemo;Ukonga, Kiwalani, Yombo Dovya, Vituka, Buza, Kivule, Kipunguni, Mwanagati, Magole, Gongolamboto, Minazini na Nyatira

Ujenzi wa nyumba ya Mapadre ulianza 2007 na kukamilika 2009 kwa nguvu za waamini wenyewe. Askofu Mkuu Mwadhama Polycarp Pengo aliamua kuitangaza Kitunda kuwa Parokia mwaka uliofuata 2010 baada ya kuona juhudi, na Pd. James Mweyunga kuwa Paroko wa Kwanza.

Ujenzi wa Kanisa kubwa la  Parokia ya Kitunda ulianza Julai 2012 na kukamilika 2018. Baada ya kuwa Parokia, Parokia ya Kitunda ilirithi vigango vya Mwanagati na Magole na baadaye kuzaa Parokia ya Kivule na Mwanagati

 

Uongozi wa Parokia
Pd. Stephano Kaombe
PAROKO
Tel : 0754-635048
Short Bio: Padri wa Jimbo la Dar es salaam
Pd. Jovin Bakekera
PAROKO MSAIDIZI
Tel : 0754-447120
Short Bio: Padri wa Jimbo la Dar es salaam

DEODATUS BALILE
MWENYEKITI,KAMATI TENDAJI, H/WALEI PAROKIA
ADOLPHINA WILLIAM
MAKAMU MWENYEKIT, KAMATI TENDAJI, H/WALEI PAROKIA
DR. EDMUND MABHUYE
KATIBU,KAMATI TENDAJI, H/WALEI PAROKIA
BIBIANA A. MALLEY
KATIBU MSAIDIZI, KAMATI TENDAJI, H/WALEI PAROKIA
JOSEPH M. MABUSI
MTUNZA FEDHAKAMATI TENDAJI, H/WALEI PAROKIA,
Pd. Stephano Kaombe
PAROKO
Tel : 0754-635048
Pd. Jovin Bakekera
PAROKO MSAIDIZI
Tel : 0754-447120
Ratiba ya Misa na Sakramenti
Day Mass Time Confession Time Other Sacraments
Monday - Friday 6:30 AM, 12:00 PM 5:00 PM - 6:00 PM Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment
Saturday 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) 4:00 PM - 5:00 PM
Sunday 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM 6:30 AM - 7:30 AM
Tusaidie Kukua: Ungana Nasi Kuitimiza Dhamira Yetu
Huduma na Vikundi
  • Kwaya ya Roho Mtakatifu: Inatoa nyimbo zenye nguvu za kumwinua Mungu na kuimarisha ibada.
  • Huduma ya Familia: Kikundi hiki kinalenga kuimarisha maisha ya kifamilia kwa maombi na mafundisho ya neno la Mungu.
  • Huduma ya Vijana: Vijana wanahamasishwa kujifunza zaidi kuhusu imani yao na kushiriki kikamilifu katika maisha ya parokia.
  • Huduma ya Upendo: Hutoa msaada wa kijamii kwa familia zenye changamoto, ikiwemo misaada ya chakula na mavazi.
Jiunge Nasi
Parokia ya Kitunda inakaribisha waamini wote kushiriki katika huduma zake na vikundi mbalimbali. Ushiriki wako utaimarisha mshikamano wa kijamii na kiimani, huku ukichangia ukuaji wa maisha ya kiroho. Jiunge na jumuiya ndogo ndogo au vikundi vya huduma ili kushiriki katika kujenga jamii yenye mshikamano wa Kikristo.
Saidia Parokia
Parokia inahimiza waamini na wadau mbalimbali kuunga mkono kazi zake kupitia michango ya fedha, muda, na vipawa. Michango yako inasaidia miradi ya parokia, kama vile misaada kwa wahitaji na kuboresha miundombinu ya parokia. Kwa msaada wako, tunaweza kuimarisha huduma za kiroho na kijamii kwa waamini na jamii kwa ujumla.
Matukio:

Coming soon...

Habari:

Coming soon...

Matangazo:

Coming soon...