Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Miaka ya 60 wakristo wa maeneo ya Mburahati walikuwa wanahudumiwa Kiroho na Parokia ya Msimbazi Msimamizi wa Kituo cha Mburahati. Huduma hizo zilikwisha mwaka 1968 kutokana na sababu za Kijografia na baadaye kuwa chini ya Parokia ya Magomeni chini Padre Oswin Baumann akisaidiwa na Padre John Manez aliyekuwa Paroko msaidizi
06/03/1972 kamati ya Jimbo iitwayo DEVELOPMENT OF RESOURCES ilikutana na kukubaliana na kupanga nyumba mtaa wa Makurumla “A” ya Utawa wa Tatu ulioko chini ya MT.FRANCIS wa Asizi kwaajili ya kituo cha ibada na Misa. Mnamo 02/07/1972 iliazimisha Misa ya ufunguzi wa nyumba hiyo wakristo wapatao 20-30 walihudhuria. Mipango ya ujenzi wa kanisa dogo Mburahati NHC ulianza (1972 na kukamilika 1974 sehemu hiyo ndio ukumbi kwa sasa. Baada ya hapo kituo au kanisa lilihama Mburahati NHC lilipo sasa. Mnamo 24/04/1974 kanisa dogo hilo lilianza kutumika rasmi.
Tar 20/04/1983 Mwadhama Kardinal Lauriani Rugambwa alibariki na kufungua rasmi jengo jipya na kuitwa Kanisa Katoliki la Familia Takatifu Mburahati. Waamini wapatao 296 walipokea Sakramenti ya Kipaimara siku hiyo. ( ili kufahamu zaidi bonyeza kitufe Historia )
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Huduma za Kichungaji: Misa za kila siku, mafundisho ya imani, semina za familia, na sala za pamoja.
- Vikundi vya Utume: Wanafunzi Wakatoliki, WAWATA, Jumuiya ya Familia Takatifu, Kwaya ya Parokia.
- Huduma za Kijamii: Huduma kwa maskini, watoto yatima, na familia maskini.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...