Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Parokia ya Bikira Maria Consolata, Kigamboni ilizaliwa kutoka Parokia ya Mt. Yosefu katika mchakato ufuatao: Kati ya miaka 1939 – 1942, Wakatekumeni kadhaa walipata ubatizo katika parokia ya Mt. Yosefu, wakristu hao waliongezeka polepole ambapo kufikia mwaka 1960 tayari kulikuwa na jumuiya kubwa yenye kaya zaidi ya waumini 30 wakisali chini ya mti wa mzambarau (wakati huo) kwenye eneo la shule ya msingi Kigamboni.
Mwaka 1969, Mkuu wa shirika la wamisionari waconsolata Padre Liyori alileta ombi kwa Mhashamu Baba Askofu Edger Marantha wa Jimbo la Dar es salaam wakati huo, juu ya kuanzisha utume wa wamisionari waconsolata eneo la Kigamboni. Baba alikubali ombi hilo. Mwaka 1970, Ujenzi wa kanisa na nyumba ya Mapadre ulianza na kukamilika mapema mwaka 1973. ujenzi huo ulifanywa na jumuiya ya waamini chini ya usimamizi wa mapadre wa Consolata, chini ya Padre Orsola ambaye alikua Paroko wa kwanza wa parokia hii na msaidizi wake Padre Julio, Imc.
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Huduma ya Vijana: Huduma hii inawalenga vijana wa parokia, kuwawezesha kushiriki katika ibada na shughuli za kijamii zinazolenga kukuza maadili ya Kikristo.
- Kwaya ya Parokia: Kwaya hii inajivunia kutoa nyimbo za ibada na kuhamasisha waamini katika ibada zao.
- Huduma ya Familia: Huduma hii inatoa msaada kwa familia zinazohitaji, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kiroho na msaada wa kifedha kwa familia maskini.
- Huduma ya Maombezi: Maombi ya parokia yanatolewa kwa ajili ya familia, waamini, na jamii kwa ujumla, huku wakikumbuka mahitaji ya kila mmoja.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...