Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Yerusalem
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
INTRODUCTION
Yerusalemu ni mji muhimu sana kwa Wakristo, kwa sababu matukio mengi muhimu ya maisha ya Yesu Kristo—mateso, kifo na ufufuko—yanahusishwa na maeneo ya mji huu. Yerusalemu ni sehemu kuu ya kutafakari historia ya wokovu.
HISTORY & SIGNIFICANCE
1. Kanisa la Kaburi Takatifu (Church of the Holy Sepulchre)
Hili ndilo eneo muhimu zaidi kwa hija huko Yerusalem, linahusishwa na: Mahali Yesu alisulubiwa, Golgotha/Kalvari, Mahali mwili wa Yesu uliwekwa kaburini na Mahali pa Ufufuko wa Kristo. Ni sehemu zinazoheshimiwa sana na Wakatoliki, kama Kalvari na Kaburi Takatifu.
2. Via Dolorosa – Njia ya Msalaba
Ni njia katika Mji wa Kale wa Yerusalemu inayohusishwa na safari ya Yesu kuelekea kusulubiwa. Ina Vituo 14 vya Msalaba (Stations of the Cross), ambavyo Wakatoliki hutumia kwa sala na kutafakari mateso ya Kristo.
3. Kanisa la Gethsemane
Liko karibu na Bustani ya Gethsemane, chini ya Mlima wa Mizeituni. Ni mahali panapohusishwa na maombi ya Yesu usiku kabla ya kukamatwa kwake. Kanisa hili ni muhimu sana kwa kutafakari mateso ya Kristo.
4. Mlima wa Mizeituni (Mount of Olives)
Ni eneo lenye umuhimu mkubwa katika Injili. Linahusishwa na; Yesu kufundisha, Maombi yake na Kupaa kwake mbinguni, kwa mujibu wa mapokeo ya Kikristo.
5. Kanisa la Kupaa Mbinguni (Chapel of the Ascension)
Eneo linaloheshimiwa kama mahali Yesu alipaa mbinguni baada ya Ufufuko. Kwa Wakatoliki ni mahali pa sala na tafakari juu ya Kristo aliyefufuka na kutukuzwa.
6. Kanisa la Mtakatifu Petro huko Gallicantu (St. Peter in Gallicantu)
Linahusishwa na tukio la Petro kumkana Yesu mara tatu, kabla ya jogoo kuwika. Ni sehemu nzuri sana kwa kutafakari juu ya toba, udhaifu wa mwanadamu na huruma ya Mungu.
7. Eneo la Ukuta wa Magharibi (Western Wall) hujulikana pia kama - Ukuta wa Maombolezo. Hili ni eneo takatifu sana kwa Uyahudi, Hata hivyo wageni hufanya hija na kupeleka maombi yao hapo.