KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Cascia (Italy)
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
40
Mawasiliano
hijaroma@darwalei.or.tz
+255 787 188 503
Eneo
Europe
Lugha
Englis Franch Italiano

Umuhimu wa Hija

Cascia

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Kashia (Cascia), ni mji uliopo nchini Italia, ni eneo lenye umuhimu mkubwa sana wa kiroho kwa sababu ndiyo mahali ambapo Mt. Ritha wa Kashia alipoishi mpaka kifo chake, na karibu na hapo ni eneo la Roccaporena, kijiji alikozaliwa mwishoni mwa karne ya 14.

Region: Cascia

HISTORY & SIGNIFICANCE

Kashia Cascia) ni mahali pa hija kwa Mt. Ritha
Umuhimu wake unatokana na matukio ya maisha na ushuhuda wa imani wa Mt. Ritha. Katika Maisha yake. Aliolewa na akapata Watoto. lakini maisha yake ya ndoa yalikuwa na changamoto kubwa.

Baada ya kumpoteza mume wake na baadaye watoto wake, aliingia katika maisha ya utawa wa Waagustino huko Cascia. Huko ndiko alikoishi maisha yake ya utawa katika monasteri ya Waagustino, na ndiko alikofia. Leo mwili wake umehifadhiwa katika Basilica ya Mt. Ritha wa Kashia, ndani ya jeneza la kioo

Mt. Ritha alikuwa mvumilivu, mtu wa msamaha, mtu wa sala na upendo, hasa katika mazingira ambayo yalionekana kuwa magumu sana kibinadamu. Mt. Rita amekuwa akiheshimiwa kama mwombezi wa mambo magumu na yasiyowezekana Hii ndiyo sababu, wengi husali Novena yake wanapokuwa na jambo ambalo wamejaribu kulitatua kwa njia mbalimbali bila mafanikio. Novena yake ni sala inayofanywa kwa kipindi maalum, mara nyingi siku tisa.na siku 3 ni za shukrani

Ili kufahamu zaidi jiunge na safari ya hija ujue mengi zaidi