Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Assisi / Mt. Clara
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
INTRODUCTION
Assisi, nchini Italia, ni sehemu ya pekee sana kwa Wakatoliki kwa sababu inahusishwa kwa karibu sana na maisha na urithi wa Mtakatifu Fransisko wa Assisi na Mtakatifu Klara wa Assisi.kupitia maisha ya watakatifu hao, maisha ya watakatifu hao yamewafanya wakuwe kiimani
HISTORY & SIGNIFICANCE
Basilica ya Mtakatifu Fransisko
– Hapa ndipo lilipo kaburi la Mtakatifu Fransisko, mwanzilishi wa Shirika la Wafransiskani. Alijulikana kwa maisha ya umaskini, unyenyekevu, upendo kwa maskini na kujali uumbaji. Basilica hiyo pia ina michoro maarufu ya maisha yake.
Basilica ya Mtakatifu Klara
– Mtakatifu Klara alikuwa mfuasi wa karibu wa Fransisko na mwanzilishi wa Shirika la Masista Waklara (Poor Clares). Kaburi lake liko katika Basilica ya Santa Chiara.
Assisi ni mahali pa hija na sala – Waamini wengi huenda huko si kama watalii tu, bali kwa hija, kutafakari, kuungama, kushiriki Misa na kusali. Mazingira ya mji huo wa kale yanafanya safari iwe na hali ya kiroho sana.
Assis ndipo alipozaliwa Mtakatifu Francis, Basilika ya Mtakatifu Clara na Mt. Mary Major eneo hili ndimo ambapo mwili wa Mt. Carlo Acutis umehifadhiwa. Kanisa la Santa Maria Maggiore pia linaitwa Santuario della Spogliazione (Sanctuary of the Spoliation). Kaburi lake liko katika upande wa kulia wa kanisa (right aisle).