KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Lourdes (France)
ENEO: LOURDES
No more photos
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
40
Mawasiliano
hijalourdes@darwalei.or.tz
+255 787 188 504
Eneo
Europe
Lugha
Englis Franch Italiano

Umuhimu wa Hija

Lourdes

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Lourdes ni mji ulioko kusini-magharibi mwa Ufaransa, chini ya milima ya Pyrenees, katika eneo la Hautes-Pyrénées. Kabla ya 1858, ulikuwa mji wa kawaida wenye historia ya kale.
Umaarufu wa mji wa Lourdes unausishwa na mtoto wa kike aitwaye Bernadette Soubirous aliyezaliwa Mwaka 1844. Familia yake ilikuwa maskini, na wakati wa ujana wake waliishi katika nyumba ndogo iliyokuwa zamani gereza, inayojulikana kama Le Cachot

Region: Lourdes

HISTORY & SIGNIFICANCE

Kinachoufanya mji wa Lourdes ujulikane duniani kote ni kutokana na historia inayoanzia Mnamo 11 Februari 1858. Wakati Bernadette akiwa na umri wa miaka 14, alikwenda eneo la Grotto ya Massabielle, hapo alimwona mwanamke mwenye mavazi meupe. Baadaye alimtambua mwanamke huyo kuwa Bikira Maria.
Kwa jumla, Bernadette alisema alikutana na huyo mwanamke mara 18, kati ya 11 Februari na 16 Julai 1858

Wakati wa tukio la 25 Februari 1858, Bernadette alielekezwa kuchimba ardhini kwenye Grotto. Maji yakatokea hapo. Baadaye chemchemi hiyo ikawa maarufu sana, na mahujaji kutoka sehemu mbalimbali duniani wakaanza kuja kwa ajili ya sala na matumizi ya maji hayo.

Tangu hapo, Lourdes imekuwa moja ya vituo vikubwa zaidi vya hija ya Kikatoliki duniani. Mamilioni ya mahujaji huenda kila mwaka, hasa kwenye Grotto ya Massabielle, Basilika mbalimbali, Misa, Rozari, Kitubio, maandamano ya Ekaristi na maandamano ya mishumaa usiku.
Kwa hiyo, kwa wanaokwenda Lourdes, ni vizuri kukumbuka kwamba hija hiyo haianzi na Basilika kubwa zinazoonekana leo, bali inaanzia kwenye maisha ya msichana maskini, Bernadette, na matukio yaliyotokea kwenye Grotto mwaka 1858

Mambo muhimu ya kutarajia ufikapo Lourdes ni haya yafuatayo;
1. Kutembelea Grotto ya Massabielle, kugusa mwamba kwa heshima, kusali na kunywa maji ya LourdesKuna
2. Misa mbalimbali kila siku, ikiwemo Misa ya Kimataifa ambayo huadhimishwa kwenye Basilika kubwa iliyoko chini ya ardhi.
3. Kusali Rozari; Rozari husaliwa kila siku kwenye Grotto.
4. Kitubio/Kuungama
Kuna Chapeli ya Upatanisho (Confession),
5. Kuoga au kufanya ishara ya maji ya Lourdes
Kuna Piscines ambapo mahujaji wanaweza kushiriki katika ibada ya maji.
6. Maandamano ya Ekaristi
7. Maandamano ya Mwanga (Torchlight/Marian Procession
8. Kuwakumbuka wagonjwa na wenye ulemavu