Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Ghuba ya Suez
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
INTRODUCTION
Ghuba ya Suez; Ni eneo muhimu na maarufu duniani kwasababu ya uwepo wa Mfereji wa Sue Canal, eneo Hili hutumika kupitisha meli kubwa duniani na chini yake kuna barabara ya magari inayopita chini ya maji kwa wasafiri wa barabara. Eneo hili limekuwa kivutio kikubwa.
HISTORY & SIGNIFICANCE
Kadiri ya maandiko, wana wa Israel walivuka Bahari ya Shamu kwa miguu baada ya Musa kunyoosha fimbo yake na maji yakagawanyika. Hayo ni matendo Makuu ya Mungu yakisimuliwa juu ya miujiza iliyofanywa na Mungu kupitia mtumishi wake Musa.
Nchini Misri kuna Ghuba Mbili, yaani (Gulf of Aqaba na Gulf of Suez). Gulf of Suez ndiyo wana wa Israel walitumia kuvukia baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Farao. Kwa kawaida ghuba ni mkondo wa Bahari ulioingia nchi kavu. Mfano wa eneo la daraja la kigamboni. Hapa ndipo Musa alinyoosha fimbo yake na maji ya Bahari yakagawanyika, tukio hili linaonyesha uwepo wa nguvu ya Mungu.
Mwisho wa mkondo wa Bahari wa Suez ndipo Waingereza walichimba na kutengeneza mfereji Suezi (Suez Canal) unaounganisha Bahari ya Shamu na ile ya Mediterranean. Kiungo hiki kilichotengenezwa na wanadamu kipo mbali kidogo kutoka mahali wana wa Israel walivukia .kwa sasa hakuna miujiza tena kama ile ya Musa kwakuwa imechimbwa barabara inayopita chini ya bahari ya mkondo wa Suez inayowezesha mabasi kusafiri chini ya bahari wakati meli zikipita juu.(Kutoka 14:15)
MUUJIZA WA MAJI MACHUNGU YA MARA
Hili ni eneo la jangwa na maji pekee yaliyopo ni kisima kilichokuwa na maji machungu japo maji hayo yalibatilishwa toka uchungu na kuwa matamu. Kwa sasa hayatumiki. (Kutoka 15:22 -27)