KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Jangwa la Sinai (Misri)
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
40
Mawasiliano
Wasiliana nasi
Eneo
Africa
Lugha
Kiingereza Kiebrania Arabic

Umuhimu wa Hija

Jangwa la Sinai

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Jangwa la Sinai lnapatikana katikati ya Elimu na Sinai. Elimu ni sehemu mojawapo katika historia ya Biblia kwani ndipo ambapo Mungu aliwalisha wana wa Israel Mana kabla ya kufika Refidimu mahali ambapo Israel walipigana na Waameleki. Waisrael walinung’unika sana juu ya Mana wakidai ni chakula dhaifu na Mungu akaamua kuwapa Kware (Ndege wa porini) ili wale nyama pia. Mambo haya yalitokea miaka 3400 ukithibitisha misha yaw ana wa Israel walivyokuwa wakitembea na Mungu

Region: Sinai

HISTORY & SIGNIFICANCE

JANGWA LA SINAI
NI eneo lisilokuwa na kitu chochote cha makumbusho lakini ndilo eneo ambapo wana wa Israel walimnung’unikia Musa kwa mara ya pili, hapa ndio sehemu walipolalamika juu ya njaa na kutamani kurudi Misri na Mungu akaahidi kuwanyeshea mikate ijulikanayo kama Mana. (Kutoka 19:4)
Wakiwa katika eneo hili walikosa maji baada ya kula nyama ya Kware wa miujiza ambao Mungu aliwapa kabla ya kumnung’unikia Musa na ndipo Mungu alipomwambia Musa agonge mwamba na maji yakatoka.
RAFEDIMU
Ni safu za milima. Awali ilikuwa nchi yenye mamlaka na utawala wake chini ya Mfalme Hagagi. Waameleki walioishi eneo hilo waliwazuia Israel wasipite na Mungu akamtuma Yoshua apigane nao. Hapo ndipo Musa alipopanda mlima na kuinua mikono juu ili Israel washinde vita. (Kutoka 17:8-12)

MLIMA SINAI
Kwa sasa mji huo umebadilishwa jjina na kuitwa St. Catherine. Mji huo una baridi kali kwakua ni jangwa na pia ni mlima. Wakati wa kuelekea kupanda mlima askari huongoza msafara sababu ya kuhofia magaidi.eneo hilo huishi pia watu wa kabila la Bedui wanaoishi milimani. Eneo hili kuna hotel moja tu inayojulikana kwa jina la Morgan Land Hotel ambayo hutumiwa na wageni wanaofika eneo hilo.(Kut 19:1-25)
MENGINEYO
• Pango la Nabii Eliya. Aliishi siku 40 wakati alipomkibia Yesebeli baada ya kuuwa manabii 400.(1 Wafalme 18; 1-8)
• Mahali ilipotengenezwa ndam ya dhahabu (Kutoka 32:19)
• Kisima ambacho Musa alikutana na Sipora alipomkimbia Farao. Sipora alikuwa binti wa Yetro. Kut 2:17
• Kichaka kilichowaka moto lakini hakiteketei (Kutoka 3:1 -15)