Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Lisbon
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
INTRODUCTION
Lisbon (Lisboa) ni eneo lenye historia ndefu sana, majengo ya kihistoria, makumbusho mengi na Mto Tagus (Rio Tejo) unaopitia kando ya jiji.
HISTORY & SIGNIFICANCE
Historia yake inaanza zamani sana: Wafoinike waliweka makazi katika eneo hilo, wakilihusisha na jina Alis-Ubbo. Baadaye eneo hilo likawa makazi ya Warumi yaliyoitwa Felicitas Julia Olisipo, kuanzia kipindi cha Warumi. Katika karne ya 8, Wamoor walifika na kulitawala jiji hilo, ambalo waliita Aschbouna.
Mwaka 1147, Mfalme Afonso Henriques, mfalme wa kwanza wa Ureno, aliliteka Lisbon kutoka kwa Wamoor. Mwaka 1255, Lisbon ikawa mji mkuu wa Ureno
Maeneo ya Kutembelea
🏰 Castelo de São Jorge; Hili ni Jumba la São Jorge, lililoko juu ya kilima cha Lisbon. Kutoka hapo unaweza kuona sehemu kubwa ya jiji pamoja na Mto Tagus. Ngome hiyo ina uhusiano mkubwa na historia ya kutekwa kwa Lisbon kutoka kwa Wamoor mwaka 1147
⛪ Sé de Lisboa; Hili ni Kanisa Kuu la Lisbon, moja ya majengo muhimu ya kihistoria ya jiji. Limejengwa katika mtindo wa Romanesque na lipo katika eneo la zamani la Lisbon. Kuna pia sehemu ya hazina na cloisters za kutembelea.
Lisbon Museum – inaeleza historia na maendeleo ya Lisbon kuanzia nyakati za kabla ya historia hadi karne ya 20. Ina vituo kadhaa, ikiwemo Pimenta Palace, Roman Theatre na Casa