KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Yeriko (Israeli)
ENEO: YERIKO
No more photos
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
30
Mawasiliano
hijaisrael@darwalei.or.tz
+255 787 188 502
Eneo
Asia
Lugha
Kiingereza Kiebrania

Umuhimu wa Hija

Yeriko

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Yeriko ni moja kati ya mji mashuhuri nchini Israel. Miongoni mwa mambo yanayofanya mji huu kuwa wa kipekee na kuvutia ni historia yake kuhusu Mkuyu aliopanda Zakayo, Chemchem ya maji (kisima cha Elisha), Mlima wa majaribu na mabaki ya ukuta wa Yeriko ya kale. Kwa wasomaji wanaofuatilia Biblia haya ni miongoni mwa mambo unayoweza kuyakumbuka.

Region: Yeriko

HISTORY & SIGNIFICANCE

Inasemekana asili ya watu wa mji wa Yeriko wailikuwa ni wa Kanaani ambao walimiliki ardhi na eneo la Yeriko. Baadaye Mwenyezi Mungu aliwapa wana wa Israel eneo la mji huo ili waumiliki. (Kum 34:3)
Ki -biblia mji wa Yeriko ulijulikana kama mji wa mitende na wenye chemchem nyingi uliopo kando ya mto Yodani. Uwapo Yeriko unaweza kutembelea maeneo yafuatayo: (Yosh: 6 )

MTI WA MKUYU UNAOHUSISHWA NA ZAKAYO
Tukio lililopata kuvutia sana na ambalo linasemwa kibilia ni lilie linalomhusu mtu aliyejulikana kwa ufupi wake wa kimo, huyu si mwingine ni Zakayo mabaye alipanda mti ili kumwona Bwana. Uwapo Yeriko utauona mti huo wa Mkuyu unaoishi mpaka hivi leo. (Luka 19:1-6). Tukio hili lilitokea miaka 2000 iliyopita.

NABII ELISHA NA CHEMCHEM YA MAJI
Moja kati ya maajabu yaliyolete msisimko mkubwa na wa kuvutia katika historia ya dunia mpaka leo, ni lile tukio lililotokea kwenye chemchem ya maji ambapo, Nabii Elisha alilalamikiwa na watu wa Yeriko ya kwamba pamoja na kuwa na mji mzuri na wakuvutia, lakini tatizo ni maji waliokuwa wanatumia yali zaa mapooza. Nabii Elisha aliyejawa na Roho Mtakatifu alimwaga chumvi katika chanzo cha maji na ndipo tatizo lilipo koma. Kwa neno lake ndio maana mpaka leo maji hayana madhara. Chemchem hiyo imehifadhiwa mpaka leo hii, na watu hufika kuiona.

MLIMA WA MAJARIBU
Yeriko ndipo ilipo mlima ule ambao Kristu alipandishwa na Roho ili ajaribiwe na ibilisi mara to baada ya kutoka mto Yodani kubatizwa na kuthibitishwa na Roho Mtakatifu kuwa ni mwana wa Mungu (Mathayo 4:8- !0 )

MASALIA YA UKUTA WA YERIKO
Ukuta huo ulibomolewa na Mungu mwenyewe kwa maandamano ya wana wa Israel ambao waliuzunguka kila siku mara moja, siku ya saba walizunguka mata saba huku wakiimba na kupiga kelele za tarumbeta na ukuta ukaanguka. Ukuta haukuwa wa kawaida, ulikuwa ngome ya kivita.
Unakaribishwa kujiunga na Hija ili ushuhudie matendo makuu ya Mungu