KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Bethlehemu (Israeli)
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
30
Mawasiliano
hijaisrael@darwalei.or.tz
+255 787 188 502
Eneo
Asia
Lugha
Kiingereza Kiebrania Arabic

Umuhimu wa Hija

Bethlehemu

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Bethlehemu ni mji wa kale sana katika Milima ya Yudea. Jina Bethlehemu maana yake ni nyumba ya mikate, jina hili lililtokana na historia ya watu wa eneo hilo kutokana na shughuli za kilimo cha ngano kama malighafi ya mkate. Bethlehemu inahusishwa na Mfalme Daudi, ambaye Biblia inamtaja kama mzaliwa wa Bethlehemu. Na pia ndio chimbuko la mapokeo ya Kikristo yanayoweka kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Region: Bethlehemu

HISTORY & SIGNIFICANCE

Bethlehemu eneo maarufu kadiri ya maandiko ya Biblia. Umuhimu wake unatokana na haya yafuatayo;

UWEPO WA KANISA LA KUZALIWA KWA YESU – CHURCH OF NATIVITY
Hili ni eneo lilipokuwa hori la kulia ng’ombe, hapo limejengwa Kanisa la Kuzaliwa kwa Yesu – Church of Nativity; Kanisa linahusishwa na mahali Yesu alipozaliwa. Ndani ya Kanisa hilo chini yake kuna Pango la Kuzaliwa Kristu (Grotto of the Nativity). Ni sehemu inayoheshimiwa sana (Luka 2:4-7) kwenye eneo hilo imebandikwa picha ya nyota yenye pembe 14 kuashiria vizazi 14 vya Israel. (Mathayo 4:17)
Kanisa lilijengwa na Mfalme Constantino na mamaye Helena 333 AD- 339 AD na Mwaka 565 Kanisa jipya la Nativity lilijengwa na Kaisari Justinian. Makanisa yote matatu kwa sasa yapo chini ya UNESCO

SHAMBA LA BOAZ - SHEPHERDS FIELD
Hili ni shamba la Boaz ambaye anatajwa kwenye Biblia kitabu cha Ruthu. Hapa ndipo Wachungaji wa kondeni walipotokewa na Malaika usiku na kupashwa Habari za kuzaliwa kwa Kristu. Shamba hilo lipo mpaka leo

KABURI LA MKE MDOGO WA YAKOBO (RAHELI)
Hili ni eneo mohawapo ambali limekuwa kivutio kutokana na historia ya Biblia kuhusu mke mdogo wa Yakobo (Raheli). Kaburi hili liko maeneo ya Wapalestina kwasababu ndipo mahali alifariki wakati wakirejea kwa toka kwa baba yake Labani wakati akijifungua mtoto wake wa mwisho aitwaye Benjamin (mwanzo 35:18-19)
Hayo ni baadhi tu ya maeneo. Unakaribishwa kufuatilia zijazo ili uweze kujifunza zaidi.