KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Nazareth (Israeli)
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
40
Mawasiliano
hijaisrael@darwalei.or.tz
+255 787 188 502
Eneo
Asia
Lugha
Kiingereza Kiebrania Arabic

Umuhimu wa Hija

Nazareth

Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

INTRODUCTION

Nazareti ni miongoni mwa miji maarufu sana nchini Israel, ulianzishwa kati ya miaka ya 2200 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo. Wakati wa kuzaliwa kwa Yesu Kristo, mji huo ulikuwa katika Jimbo la Galilaya, kwa sasa ni mji Mkuu katika Wilaya ya Kaskazini. Mji huu una kilometa za mraba 14 na mita 347 kutoka usawa wa bahari

Region: Nazareth

HISTORY & SIGNIFICANCE

Sifa kubwa ya mji wa Nazareti ni kuwa, ndipo mahali Yesu alilelewa na Maisha yake ya kawaida yalikuwa Nazareti kabla ya kuanza huduma. Nyumba ambayo Yesu aiishi bado ipo mpaka leo.
Maeneo muhimu kwa wanaoenda kwaajili ya hija katika mji wa Nazareni ambayo hupaswi kuacha kufika ni haya yafuatayo;

KANISA LA TANGAZO (THE CHURCH OF ANAUNCIATION); Hapa ndipo mahali patakatifu panapohusishwa na Tangazo la Malaika Gabrieli kwa Bikira Maria. Katika sehemu ya chini kuna Grotta ya Annunciation inayoheshimiwa sana. Eneo hilo limejengwa kanisa ili kulinda kumbukumbu za eneo hilo. (Luka 1:26 -38)

SYNAGOGUE CHURCH OF NAZARETH : Sinagogi ni nyumba ya ibada za dini ya Kiyahudi ambayo ilitumika kufundishia Watoto si kuabudu pekeyake. Wakati huo hapakuwa na makanisa. Hata Yesu wakati wa utoto wake alikuwa akiingia kwenye Sinagogi la Nazareti ambalo baadaye ndilo aliloingia kusoma chou cha Nabii Isaya (Luka 4:16 -19)

KISIMA CHA MAJI ALICHOCHOTA BIKIRA MARIA: Eneo hilo kwa sasa limehifadhiwa kwa miundombinu ya hali ya juu kwaajili ya kuwapatia maji Wayahudi

KIWANDA CHA USEREMALA CHA YOSEFU (BABA MLEZI WA YESU) ; Hiki kilikuwaa ni kiwanda cha kuranda mbao ambacho Baba Mlezi wa Yesu alikimiliki. Eneo hili lmehifadhiwa vyema ijapo kiwanda chenyewe hakipo kwa sasa. Eneo hili kibiblia ni ushuhuda tosha wa Maisha ya Yesu.

ENEO LA MLIMA AMBAO WALIJARIBU KUMUUA YESU
hapa kwa kadiri ya mwandishi Dk. Luka anaeleza kwa kina kisa cha Wayahudi kujaribu kumuua kwa kumsukuma ili aanguke kutoka kilele cha mlima lakini akapita katikati yao akaondoka wasiweze kumuua. mlima huo upo nje kidogo ya mji wa Nazareti. mwinuko wake ni futi 1296 au mita 395. (Luka 4:29 -30)