Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Kapernaum
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
HISTORY & SIGNIFICANCE
Jina Kapernaum limetokana na majina mawili Kafr Naum, yaani Kijiji cha Naum. Huyu naum alikuwa Nabii wa Mungu aliyetumwa kwenda kuhubiri katika taifa la Ninawi Miaka 150 baada ya Yona kutumwa huko akagoma hadi Mungu alipo mpeleka huko kwa nguvu akiwa tumboni mwa Samaki.
Kapernaum ni miongoni mwa miji ya kale ambayo Yesu Krisu alifanya huduma huko. Kaprenaum kilikuwa ni Kijiji cha wavuvi kaskazini mwa ziwa Galilaya. Kijiji hiki kilidumu takribani karne 11 baada ya Kristu kabla ya watu wa Kijiji hicho kutawanyika maeneo mengine kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyo hatarisha Maisha yao.
Mji wa Kapernaum unajulikana kama mji wa Yesu (City of Jesus) kwa miaka mitatu na nusu ya huduma yake wakati akiishi humo. Muhimu katika mji huo ni ; Nyumba aliyokuwa akiishi Mtume Petro ambayo Yesu aliingia na kumponya mkwewe Petro.(Mathayo 8:14–15).
Katika mji huo, ndipo Yesu alimponya mwenye kupooza aliyeshushwa kupitia paa ili afike alipokuwapo Yesu. Haya mojawapo ya miujizi iliyowahi kutokea maeneo ya Kapernaum (Marko 2:1–12).
Nyumba hii baadaye iligeuzwa Kanisa baada ya Kristu kupaa Mbinguni, hii ni baada ya dini ya ukristu kuanza. Hapo ndipo Kanisa la kwanza kuanzishwa eneo la Kapernaum