KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Hija Nje ya Nchi
Hija ya Israeli

Israel ni taifa lenye hifadhi ya shuhuda nyingi za kiimani yanayotajwa Ki- Biblia, kabla, wakati na baada ya kuja Kristu. Maeneo hayo yanasimama kama lango la imani kwa wakristo duniani kote. Maelfu ya wageni huenda kila mwaka kwaajili ya hija.

Maeneo Matakatifu ndani ya taifa la Israel na Jirani yana umuhimu mkubwa sana kwa Wakristo kwasababu mengi yanahusishwa na matukio ya mbalimbali kuhusu asili ya maisha ya imani, yaani kuja kwake Kristu na safari ya ukombozi wa dunia ikihusisha mateso, kifo na ufufuo wa Yesu Kristo ambao ndio wokovu wa wanadamu. Maeneo yanayotajwa ni ;Yerusalemu, Bethlehemu, Nazareth, Kana, Galilaya, Yodan na Misri. Nakushauri ufuatilie na pia unakaribishwa katika hija zinazoendele.

Mkristo anapotembelea maeneo hayo si tu anafanya utalii bali kutumia safari hiyo ya hija kuunganisha maandiko na maeneo ya Ki- historia katika kujifunza, kutafakari juu ya maisha yatakayo mjenga kimani.