KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Hija Nje ya Nchi
Hija ya Misri

Misri ni moja kati ya nchi zinazopatikana katika bara la Africa. Makao Makuu yake yapo Cairo. Lugha ya mawasiliano inayotumika ni Kiarabu na Kiingereza kwa asilimia ndogo. Jamii ya watu wa Misri ni waamini wa dini ya kiislamu na pia ni mji wenye historia

Nchi ya Misri inapakana na Libya, Sudani, Israel na ukanda wa Gaza upande wa Mashariki ya Kati. Ni mji wenye historia nyingi za kale.  Ukilinganisha na nchi nyingine zilizoko barani africa, Misri ni nchi mojawapo iliyopiga hatua kubwa kimaendeleo, kiuchumi na hata ki-miundombinu. utalii ni moja ya vyanzo vikubwa vya mapato kutokana na uwepo wa vivutio vingi.

Kinachofanya nchi ya Misri kuwa ya kipekee ni Pamoja na vivutia vyenye historia ndefu za watawala wa wakati huo yaani Mafarao na makaburi ya Mafarao yaani Pyramids, Makubusho ya kale, mto Nile, mfereji wa Suez Canal, Mlima Sinai na historia mbalimbali zinazohusishwa na Biblia kuhusu Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu.

Nakukaribisha uweze kufatilia safari za hija ili kujionea mambo mbalimbali