Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Ureno iko kusini magaharibi mwa Ulaya kwenye Rasi ya Iberia, inapakana na Hispania (Spain) na upande wa mashariki na kaskazini na huku upande wa magharibi ni bahari ya Atlantic. Mji Mkuu wa Ureno ni Lisbon, pia kuna miji mingine mikubwa kama Porto, Braga, Coimbra na Faro.
Shughuli kuu ni Utalii, ule wa kawaida na wa kidini. Shughuli nyingine ni kilimo, Uvuvi, viwanda na Biashara
Ureno ilipata umaarufu zaidi kutokana na kuwepo kwa hija katika mji wa Fatima, ambapo waamini wengi wa dini ya katoliki kutoka sehemu mbalimbali za dunia hufika katika mji huo kwaajili ya kufanya hija katika maeneo alipo tokea Bikira Maria.
Fatima ipo Ureno na ni moja ya vivutio muhimu sana vya hia za kikatoliki duniani ikihusishwa na matukio makubwa ya mwaka1917 ambapo watoto watatu wachungaji -Lucia, Fransisco na Yasinta walitokewa na Bikira Maria katika eneo la Cova da Iria na kanisa kutambu rasmi matukio hayo mwaka 1930