KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Eneo la Hija
Eneo la Pugu (Dar es Salaam)
Miezi ya Hija
Wasiliana nasi
Gharama
Wasiliana nasi
Washiriki
Wasiliana nasi
Mawasiliano
0717165024
Eneo
Dar es Salaam
Lugha
Kiswahili Kiingereza French

Umuhimu wa Hija

Pugu

Hija ni tendo la imani, ni safari ya kiroho ya kukufanya kujiweka karibu na muumba, kwa kufanya toba, mafungo, ibada na tafakari juu ya mamba mbalimbali ya kiroho ili kujiweka katika hali ya unyoofu.

Mahitaji ya Waombaji

  • Fomu ya Usajili
  • Chanjo zinazohitajika
  • Malipo ya gharama za safari

HISTORY & SIGNIFICANCE

Eneo la Pugu hapa Dar es Salaam lina historia pana na pia umaarufu mkubwa katika nchi ya Tanzania ikihusishwa na mambo yafuatayo;
Pugu ina historia ya Wamisionari Wabenediktini waliofika mwaka 1888 kwaajili ya kueneza injili ambao baadhi yao waliuawa mwaka 1889. Kituo kilianzishwa kama kumbukumbu ya wamisionari hao, ambao wamezikwa katika kituo cha hija pugu. Sambamba na hilo wako viongozi mashuhuri waliozikwa hapo akiwemo Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyezikwa tarehe 28 Februari 2026, Mnsg. Deogratias Mbiku na wengine.

Pugu ni kituo cha hija na ibada: Waumini hufika kwa ajili ya sala, misa, tafakari na maadhimisho mbalimbali ya Kikanisa mfano. Siku ya Wafia dini, Kutukuka kwa Msalaba, Sikukuu ya Mt. Yosefu, Biblia ya Ardhini, njia ya Msalaba, Semina n.k. pia lipo Kanisa la Parokia ya Pugu.

Eneo la Pugu linahusishwa pia na historia ya elimu kupitia Shule ya Pugu na matukio muhimu ya historia ya Tanzania. Hapa tunaangazia Shule ya Pugu (zamani St. Francis College) ina nafasi muhimu katika historia ya elimu Tanzania, hasa kwa sababu zifuatazo:
Ni moja ya shule kongwe: Ilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1948 na ilianza rasmi mwaka 1950. Awali ilianzishwa na wamisionari weupe, ( White fathers) na baadaye ilikabidhiwa kwa serikali na kubadilishwa jina kuwa Pugu Secondary School mwaka 1967. Uhusiano uliopo kati ya serikali ya Tanzania, wamisionari na shule ya sekondari ya Pugu unatokana na yafuatayo;
Mwalimu Julius K. Nyerere alifundisha hapo masomo ya Historia, Kiingereza na Kiswahili wakati ikiitwa St. Francis College Pugu, kuanzia 1952 hadi 1955. Hivyo, shule hii inahusishwa moja kwa moja na historia ya mwalimu aliyekuja kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika.

Ilikuwa shule ya kiwango cha juu wakati wa ukoloni: St. Francis College ilikuwa miongoni mwa shule zilizochagua wanafunzi waliofanya vizuri kutoka maeneo mbalimbali ya Tanganyika. Imezalisha viongozi wengi mbalimbali wa Tanzania, akiwemo Benjamin William Mkapa, ambaye baadaye alikuwa Rais wa Tanzania, pamoja na viongozi wengine wa kitaifa.

Kituo cha hija Pugu ni sehemu ambayo pia huandaliwa matukio ya kidini na kijamii mfano Pugu Marathon kwaajili ya kuchangia shughuli za uinjilishaji na hivyo kuendelea kuwavutia walio wengi na kuwa maarufu zaidi.
Eneo la kituo cha hija pugu ndipo Kanisa Kuu mbadala litajengwa yaani Theotokos, hii ni kutokana na tamko la Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwaichi alilolitoa siku ya Mavuno kijimbo huko Gezaulole 2025 kwa mara ya kwanza, ambapo baadaye alitangaza kuwa ujenzi huo kuhamia pugu.

Kwa hiyo, Pugu ina uhusiano mkubwa na Wamisionari, elimu Tanzania na viongozi walioshika madaraka ya nchi