Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Umuhimu wa Hija
Saint Joseph Cathedral
Safari hii ni fursa ya kipekee ya kiroho kwa waumini.
Mahitaji ya Waombaji
- Fomu ya Usajili
- Chanjo zinazohitajika
- Malipo ya gharama za safari
HISTORY & SIGNIFICANCE
Ni Kanisa la hija lililopo Jimbo kuu la Dar es Salaam. Kinachofanya kuwa la kipekee ni kutokana na historia yake.
Ni Kanisa Kongwe ukilinganisha na makanisa mengine yaliyopo katika Jimbo la Dar es Salaa. Limekuwa Parokia mwaka 1889, kufikia mwaka 1953 yaani miaka 64 baadaye, bado Dar es Salaam ilikuwa na Parokia moja tu ambayo ni Mt. Yosefu.
Ndilo Kanisa Kuu la Kiaskofu, hadhi ambayo ilipata 1953 Machi 23. Kanisa Kuu limepata bahati ya kuwa na Maaskofu wa Wakuu wanne mpaka sasa. (Mhashamu Edga E. Maranta, Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwaichi ambaye ndiye Askofu Mkuu wa Jimbo kwa sasa)
Ujenzi wake ulifanywa na Wajerumani kuanzia 1897-1889 kwa ujuzi mkubwa. Uwepo wake umekuwa ndio sababu ya kuzaliwa Parokia nyingine zilizopo Jimbo la Dar es Salaam kufikia 170 na Parokia Teule 23. Dekania 16 kufikia Agosti 2026.
Kanisa kuu la Mt. Yosefu lina utajiri mkubwa wa kuwa na maeneo mbalimbali kwaajili ya sala na huduma nyinginezo kama nafasi ya kushiriki Misa, Sakramenti ya Kitubio, Mafungo, Kuabudu Ekaristi, sala za Rozali kwa Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu. Yapo mafundisho kwaajili ya Watoto na watu wazina.
Zipo pia kumbukumbu mbalimbali zilizohifadhiwa ndani ya Kanisa ikiwemo historia ya Kanisa Kuu la Mt. Yosefu tokea kuzaliwa kwake ikihusisha historia za jimbo la Dar es Salaam na Viongozi
Ndani ya eneo la St. Joseph Cathedral yapo maeneo mbalimbali ambayo yatakuweka karibu na Mungu kwa kupata fursa ya Kuabudu Ekaristi Takatifu kadiri ya muda wako, kwani pako wazi masaa 24. Ipo Grotto ya Mama Bikira Maria na Kapela ya Mt. Yoseph. Ndani ya Kanisa Kuu kuna (Chapels) na pia ndani ya Kanisa umehifadhiwa mwili wa Askofu Shahidi wa kwanza Jimbo la Dar es Salaam Kassian Spiess, na utapata nafasi ya vitabu vya kumbukumbu mbalimbali kikiwemo kiti alichokalia Baba Mt. Yohane Paul wa II. wakati wa ziara yake
Kwa maelezo zaidi tembelea Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu kwaajili ya huduma mbalimbali za Kiroho na kujifunza juu ya mambo mbalimbali