Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Jiji la Dar es salaam ni eneo mojawapo lililopiga hatua kwa maendeleo makaubwa ya kiimani kwa wakristo wakatoliki, ambapo kwa sasa, katika Jimbo la Dar es Salaam pekee, zipo Parokia kamili 170 na Parokia Teule 23. haya ni mafanikio makubwa sana.
Yapo maeneo mbalimbali ndani ya Dar es Salaam na ukanda wa Pwani maalumu kwaajili ya; Hija, Mafungo, Ibada, tafakari, kusikiliza Neno la Mungu na pia Sakramenti ya upatanisho inapatikana ili kuwaweka waamini vyema katika mahusiano na Mungu. Yapo Maeneo mbalimbali yaliyoandaliwa kwajili hayo, baadhi yake ni haya yafuatayo;
Kituo cha hija Pugu, Bagamoyo, Saint Damiano au Padre Pio Shrine, Konsolata Mission, St. Joseph Cathedral, Gaspar De Bufalo na mengineyo. wote mnakaribishwa.