Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Utume huu ulianzishwa mwaka 1922 huko Ulaya (Austria). Hata hivyo utume huu haukuwa na nguvu sana hadi mwaka 1947 wakati Aksio Katoliki ilipofanya Jubilee ya miaka 25 na kufanya mkutano maalum. Wajumbe walioshiriki katika mkutano huo walishauriana kuunda kamati maalum ya kuandaa katiba rasmi. Mwaka 1948, kamati hiyo ilianza kushughulikia katiba.Mnamo tarehe 15 hadi 17 Agosti 1950 Baraza kuu la kwanza la Kimataifa la Wanaume Katoliki (International Council of Catholic Men) lilikutana huko VATICAN. Wakati huo Baba Mtakatifu Papa Pio wa XII aliidhinisha utume huu na kuuita "UNUMONES" kama rejeo la Injili ya Yohana 17:22 ............" Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja"Papa Pio XII aliteua utume huu uwe na Makao Makuu yake Vatican na ndiyo utume pekee wenye Makao Makuu yake VATICAN. Baadaye utume huu ulianza kuenezwa sehemu nyingi Ulimwenguni na hasa Ulaya. Hivyo ulionekana umuhimu wa kuuneza utume huu katika sehemu nyingine na Afrika ikiwa mojawapo.
AFRIKA:Kufuatia hoja hiyo ya kuanzisha utume huo Afrika, Viongozi wa Baraza la Kimataifa la Wanaume Katoliki (International Council of Catholic Men) I.C.C.M waliitisha kikao chao huko Nairobi tarehe 14 hadi 16 Agosti, 1983. Wakati wa mkutano huo mada nyingi zilitolewa. Maaskofu wengi kutoka Afrika kama vile Askofu Peter Dery (Jimbo la Tamare - Ghana) Askofu Silas S. Njeru (Jimbo la Meru - Kenya) Bwana Lazarius Masipeta (Kutoka Zambia) na Padri Joseph Osei (Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu wa Africa na Madagascar (SECUM). Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Walei kutoka Tanzania, hapo ndiyo vuguvugu la kuanzisha utume lilipoingia Tanzania.
TANZANIA: Mwaka 1985 utume huu ulianzishwa kwa mara ya kwanza katika jimbo la Bukoba. Mwaka 1986 mwezi Septemba utume huu ulianzishwa katika jimbo kuu la Dar es Salaam.Mpaka sasa Majimbo yalioanzisha Utume huu ni Bukoba, Geita, Dar es Salaam, Mwanza, Kahama, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Morogoro, Arusha, Tanga, Songea, Lindi, Iringa, Mbeya na Kilimanjaro
- Kuwaunganisha wanaume Katoliki wote wenye nia, mori na ari ya kulitumikia Kanisa kwa kupitia vipawa vyao
- Kuhifadhi, Kuimarisha na kulinda imani ya Kikatoliki na kuendeleza elimu na mafunzo ya dini
- Kushirikiana na vyama vingine vya kitume na mashirika mengine ya kikatoliki yaliyo ndani na nje ya Tanzania.
- Kukuza mshikamano kati ya wanachama kwa kushirikiana katika shughuli za kiroho na kijamii
- Kujishirikisha na vyama vingine vya kiroho
- Email : uwakadsm@gmail.com
- Address : S.L.P. 167, Dar es Salaam
Warning: Undefined variable $thumbnail_directory in /home2/wajida/public_html/vyama-detail-parish.php on line 464
Deprecated: is_dir(): Passing null to parameter #1 ($filename) of type string is deprecated in /home2/wajida/public_html/vyama-detail-parish.php on line 464
Warning: Undefined variable $thumbnail_directory in /home2/wajida/public_html/vyama-detail-parish.php on line 465
Deprecated: mkdir(): Passing null to parameter #1 ($directory) of type string is deprecated in /home2/wajida/public_html/vyama-detail-parish.php on line 465
Warning: mkdir(): Invalid path in /home2/wajida/public_html/vyama-detail-parish.php on line 465
·
- Misa za Umoja: Wanachama hukutana mara moja kwa mwezi kushiriki
misa maalum kwa ajili ya maombi ya wanaume.
- Mafunzo ya Maadili na Uongozi: Semina zinazoelimisha wanachama kuhusu uongozi wa
kiroho, maadili, na jukumu la wanaume katika jamii.
- Huduma kwa Jamii: Kushiriki katika shughuli za kijamii kama
kusaidia wasiojiweza, kutoa misaada, na kufanya usafi wa mazingira.
- Mikakati ya Malezi ya Familia: Programu za kutoa mafunzo ya uhusiano bora wa
kifamilia na kuwajengea wanaume misingi bora ya maisha ya ndoa.
- Mkutano
wa Mwezi: Hufanyika
kila mwezi kujadili masuala ya maendeleo ya umoja na kupanga shughuli za
baadaye.
- Mkutano
wa Kanda: Wanachama
kutoka kanda mbalimbali hukutana kila robo mwaka kwa mafunzo na
kubadilishana uzoefu.
- Mkutano
Mkuu wa Mwaka: Hufanyika
mara moja kwa mwaka kujadili mafanikio, changamoto, na kuweka mikakati ya
mwaka ujao.
Kuwa mshirika wa Shirika la Kimisionari ni njia ya kuridhisha ya kutumikia Kanisa na jamii yako. Iwe unahisi wito wa kuongoza, kutumikia, au kuimarisha safari yako ya kiroho, kuna nafasi kwa ajili yako katika mojawapo ya mashirika yetu. Wasiliana nasi leo ili kujua zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kujiunga.
- Jinsi ya Kujiunga:
Kwa maswali kuhusu uanachama, tafadhali wasiliana na vyama@darwalei.or.tz