Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Kanisa la Mt. Yosef lilipandishwa hadhi ya kuwa Parokia 1889 likiwa ni Kanisa pekee kabisa kuwa Parokia katika Jimbo la Dar es salaam. Juhudi kubwa za ujenzi wa Kanisa la Mt Yosefu zilifanywa na Padri Maurus Hartman. Miongoni mwa alama zilizoachwa na P, Maurus Hartmann kama sehemu ya juhudi zake zinazoonekana mpaka leo ni ujenzi wa Kanisa Kuu la sasa la Mt. Yosefu.
Kiwanja kilitolewa na serikali ya kikoloni kwa wamisionari Tarehe 29 Julai.1896 pale liliposimama kanisa hivi sasa. Ramani ya kanisa ilichorwa na Arkitekti Schurr kutoka Munich Tar 2 Julai.1897.
Jiwe la msingi liliwekwa tarehe 13 Machi 1898 na Bwana Liebert aliekuwa Gavana wa Afrika Mashariki ya Kijerumani [Deutsch Ostafrika] - SL. Tarehe 4 Februari 1903 Kanisa lilibarikiwa na Padre Thomas Spreiter O.S.B,
Altare ya kwanza ililetwa ikiwa ni zawadi kutoka jumuiya ya Wagoa . Altare kubwa ya mbele ilitoka Ujerumani ikiwa ni zawadi toka kwa Kaisari wa Ujerumani maarufu Caesar Wilhelm II. Kuwekwa Altare kulifuatiwa na tukio lingine muhimu tarehe 15 Octoba 1908, ambapo Askofu Thomas Spreiter O.S.B alitabaruku Kanisa na Altare.
| Day | Mass Time | Confession Time | Other Sacraments |
|---|---|---|---|
| Monday - Friday | 6:30 AM, 12:00 PM | 5:00 PM - 6:00 PM | Baptisms: Saturday 10:00 AM, Weddings: By Appointment |
| Saturday | 7:00 AM, 5:00 PM (Vigil) | 4:00 PM - 5:00 PM | |
| Sunday | 7:00 AM, 9:00 AM, 11:00 AM | 6:30 AM - 7:30 AM |
- Huduma za Kichungaji: Mafundisho ya imani, misa za kila siku, na misa za kijumuiya.
- Vikundi vya Utume: Vijana wa Kikatoliki (VIWAWA), Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA), Baraza la Walei, na Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo (Small Christian Communities).
- Huduma za Kijamii: Msaada kwa maskini, huduma kwa wagonjwa, na programu za maendeleo ya jamii.
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...
Coming soon...