Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
Praefectura ya Dar es Salaam ilionekana kukua kimaendeleo na kiimani. Baba Mtakatifu alimteua Padre Kassian Spiess kuwa Askofu wa Jimbo Dar es Salaam Tarehe 15 Septemb.1902 Katika kipindi hicho, watu wengi walizidi kulipokea Neno la Mungu ambalo lilionekana kushika kasi sana na kutoa matunda mazuri. Idadi ya Wakristo ilizidi kuongezeka, mfano wakatekumeni na watoto pia. Mahitaji ya kupeleka shughuli za Kichungaji yakaongezeka maeneo mbalimbali ili kuchochea mwamko wa Injili. Kwahiyo, huko Roma haja ya kuinua cheo cha Praefectura ya Dar es Salaam na kuwa Vicariate ilionekana kuwa jambo la msingi sana, Dar es salaam na huko St. Ottilieni Ujerumani. baada ya kuinuliwa hadhi ya Dar es Salaam kuwa vicariate Baba Mtakatifu alimteua Padre Kassian Spiess kuwa Askofu wa Jimbo Dar es Salaam Tarehe 15 Septemb.1902 Tar 07Julai.1903 Askofu Kassian Spiess alifika Dar es salaam akitokea St. Ottilien na kupokewa kwa shangwe.
Mnamo tarehe 21 Agosti,1905 palitolewa taarifa ya kuwepo vita ukanda wa Pwani eneo la Umatumbi ambayo vilisababisha hata wazungu kuuwawa.
Inasemekana kuelekea tar 12 na 13 Agosti 1905 wanamapinduzi wa vita vya maji maji walifanya mashambulizi na kuwaua watu, Akiwa safarini kurudi Kilwa mjini alivamiwa na kikosi cha Wangindo wanamapinduzi wa maji maji ambao walimchoma mkuki na kupoteza maisha. Miongoni mwa walio uwawa ni Sr. Kordula, Sr. Felista na Br. Andrea walichomwa mikuki. Mwingine Br. Gabriel alipigwa risasi na baadae mkuki. Kijana Bernhard alitoa taarifa kw kikosi cha maaskari Kilwa. Tar 17 Mei.1905 kikosi kilizika maiti, lakini baadae yalichimbuliwa na kupelekwa Dar es Salaam na kuzikwa kwa heshima katika Kanisa Kuu la Mt. Yosef tarehe 28 Desemba,1905. Askofu Kassian anakumbukwa kama shahidi aliyemwaga damu kwaajili ya Injili.
Katika kazi zake za kiutumishi, Askofu Kassiani alijituma bila kujibakiza, alitembelea mision zote za Jimbo la Dar es salam akitoa Sakramenti kwa waamini, alitembelea shule akikagua na kuonana na Waalimu pamoja na kujua changamoto zilizoko, alishirikishana na kujadili na mapadre mambo mbalimbali yahusuyo Kanisa na jamii na kufikiri namna ya kupata majengo mapya kwaajili ya maendeleo ya kazi za misioni. Atakumbukwa daima daima kama mpigania imani, apumzike kwa amani.