Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
Mhashamu Edgar Aristed Maranta alizaliwa 9 Jan 1897, Poschivo, Switzerland, alipata upadrisho 06 Apr 1924 Alikuwa Mkapuchini, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam 27 Machi 1930 [Vicar Apostolic].
Aliwekwa wakfu Tarehe 17. 08. 1930 akiwa Askofu wa Jimbo la Dar es salaam. Katika kipindi cha uongozi wake, yaani miaka 23 baadae, Tarehe 25 Machi, 1953 Jimbo Kuu la Dar es Salaam lilizaliwa, Mhashamu Edga Aristide Maranta, OFM Cap akapewa heshima ya kuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Wakati huu Jimbo likiwa linahudumiwa na Wamisionari makapuchini wa Jimbo la Uswisi. 19 Desemba 1968 alistahafu Uaskofu Mkuu wa Jimbo. 29 Januari, 1975 alifariki dunia
Majukumu ya Kiutawala.
Alifanya juhudi kubwa sana katika kuhakikisha anajenga miundombinu bora ya Kanisa.
1932 Pugu ilipata kanisa dogo la Mt. Fidelis. 1934 Nyumba ya kupumzikia masista wa mjini ilijengwa pia.
Mwaka 1948, Padre Konradin Niederberger mtaalamu wa usanifu majengo alihamia Pugu na kuanza zoezi la upimaji wa viwanja, kuchora na kusimamia kazi ya ujenzi wa shule ya sekondari kidato cha tano na sita huko Pugu kwa ajili ya Wanafunzi wakatoliki watakao andaliwa kujiunga na Chuo Kikuu, hii ni kufuatia wazo lilitolewa na Maaskofu wa Tanganyika wakati wa mkutano wao 1946 huko Tabora. Miongoni mwa waaalimu, Julius Kambarage Nyerere alikuwepo pamoja na wengine kutoka Holy Ghost Fathers. Nyumba ya upande wa chini ya Masista ilibadilishwa na kuwa zahanati kwa ajili ya wanafunzi wa chuo.