KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Vyombo Vya Habari
Habari na Matangazo
NEWS
News
Deprecated: strtoupper(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home2/wajida/public_html/news-detail.php on line 235
By Amina Kwale
Kanisa Kuu Mbadala (Theotokos) Sasa Kujengwa Pugu

Tarehe 25 Novemba 2023, kwa mara ya kwanza katika  Jimbo Kuu la Dar es Salaam iliadhimishwa misa ya shukrani katika Viwanja vya Gezaulole eneo la Kigamboni, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi aliongoza adhimisho la misa takatifu, miongoni mwao akiwepo Askofu Msaidizi, Mhashamu Henry Mchamungu na Mhashamu Stephano Musomba ambaye kwa sasa ni Askofu wa Jimbo jipya la Bagamoyo

Askofu Mkuu alitangaza rasmi kuhusu mpango wa kuwa na Kanisa Kuu mbadala litakalojulikana kwa jina la Bikira Maria Mama wa Mungu yaani (Theotokos).

Halikadhalika katika mkutano na viongozi wa Halmashauri Walei Jimbo la Dar es Salaam uliofanyika Tar 24 Februari 2024 Ukumbi wa Kardinal Adams Msimbazi, Askofu Mkuu alisema, “Agenda kuhusu kuwa na Kanisa mbadala si mara ya kwanza kuzungumziwa alisema mpango huu unamisingi yake ifuatayo;

Alisema "Jimbo la Dar es salaamu tayari lina Kanisa Kuu ambalo la Mt. Yosefu, ambalo lina miaka 123 tangu lilipo jengwa. Lilijengwa na watawa Wabenedickitini toka Ujerumani, na fedha zilizotumika zilikuwa za wakristu wa Ujerumani, lilipokuwa linajengwa, Dar es salaam ilikuwa na wakristu 248, na sasa kuna Wakatoliki zaidi ya milioni mbili. Lilipojengwa liliaminika kukidhi mahitaji na kwa miaka mingi. Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu lina uwezo wa kukalisha watu vyema 500. Miaka 25 iliyopita, Dar es salaamu ilikuwa na Parokia 25 tu, kwa sasa zipo parokia 162 zilizo kamili na 25 teule. japokuwa kufikia Novemba 2024 idadi ya Parokia imeongezeka kufikia 167 na Parokia Teule 24

Aliendelea kusema, wa muda mrefu sasa changamoto Imekuwa ni eneo la kufanyia matukio ya kijimbo, kwa sasa hata Msimbazi hapatoshi tena.

Eneo la Gezaulole lina hekari 24.8 limenunuliwa kwaajili ya maadhimisho ya kijimbo, hivyo ni muhimu kupafanya pawe na sura inayobeba Jimbo. Uzio, kisima kirefu cha maji chenye ujazo wa lita 12,000 vimeshawekwa.

Linaitwa Kanisa Kuu Mbadala kwasababu historia itaendelea kubebwa na Mtakatifu Yosefu ambalo litabeba matukio madogo madogo ya Kijimbo.

Mpango wa ujenzi umeshirikisha makundi mbalimbali Pd. Rimisho na timu yake ya wasanifu majengo waliandaa michoro, wadau mbalimbali wameshirikishwa wakiwemo maaskofu, mapadre na walei. Amesema Jengo litakuwa na uwezo wa kubeba watu 9366, urefu ni mita mraba 13,000. Pia nafasi ya kutosha imeachwa kwaajili ya shughuli zingine ikiwemo maadhimisho yazidiyo zaidi ya watu 10,000. Askofu Mkuu alisema, Mradi   huu utamshirikisha kila mtu.

Kila mbatizwa ameombwa kuchangia shilingi 2,000 kwa kipindi cha miaka 4 na sehemu ya bajeti ya Jimbo itatengwa kuchangia ujenzi, “shughuli za lazima tu ndio zitafanyika kama vile ujenzi wa makanisa, ununuzi wa maeneo na kusaidia parokia tegemezi kama 20” alisisitiza Askofu Mkuu na kuwaomba Wakristu wenye uwezo na nafasi kuchangia kwa namna ya pekee,  na kwamba kila parokia iandae majina ya watu watakaochangia".

Askofu Mkuu alisema, ‘’ombi la kukutana na Halmashauri walei ni namna ya kuratibu upatikanaji wa fedha kwa kila mbatizwa kiparokia kwa nmna ifaayo”.

Ulitolewa mwongozo kuhusu muda maalumu wa uchangiaji ambao ni mwezi wa tano (5) na  michango kuwakilishwa kufikia Tarehe 26 Mei Sherehe ya Utatau Mtakatifu.

Kwa sasa ujenzi huo umepangwa kufanyika kituo cha hija Pugu badala ya Gezaulole