Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
Baba Mt. alimteua Padre Thomas Spreiter kuwa Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam Tarehe 13Machi, 1906 miezi michache baada ya kifo cha Askofu Kassian Spiess. Alipata Daraja ya Uaskofu Tarehe 01 Mei.1906 na Askofu wa Augsburg huko St. Ottilien Ujerumani. Alitoka katika shirika la Wabenediktini wa St. Ottilien baada ya utawa huo kuanzishwa 1885. Alizaliwa Tar 28 Desemba,1865, baada ya kupata upadrisho 1897 aliteuliwa kuwa wakili wa mkuu wa ushirika. 1900 aliruhusiwa kwenda mision akakaa zaidi dar es salaam.
Askofu Spreiter aliamini vita vya maji maji vilisababishwa na siasa ya ukoloni wa Wajerumani. Juni 1906 Askofu Spreiter aliaga St. Ottilien akipitia Rome kuomba baraka ya Baba Mtakatifu Pio X. alipokelewa kwa heshima, alimwomba pia Baba Mtakatifu kubadili jina la Vikariatus ya Sanguebar (Zanzibar) ya Kusini liwe Vikarieatus ya Dar es Salaam.
Baada ya kushika wadhifa wa uaskofu, hakuchelewa kuanza kutekeleza majukumu yake ya kichungaji. Kuhusu shule, ndiye aliyependekeza juu ya uwiano katika shule za misioni kuweza kushindana na shule za serikali.
Kama hatua ya kwanza Askofu alijadiliana na waalimu wa shule za serikali na maofisa elimu kuhusu muhtasari ya mafundisho ya shule. alikutana na Gavana akapatana naye kujenga uhusiano bora kati ya misioni na Serikali.