KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Uongozi
Utawala & Utendaji

   "Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu 

Mwadhama . Polycarp Kardinal Pengo
Askofu Mkuu Mstaafu
Jimbo Kuu la Dar es Salaam

01 January 1992 - August 2019

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alizaliwa katika kijiji cha Mwazye kilichopo takribani kilometa 75 Kusini mwa mji wa Sumbawanga katika wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa uliopo Kusini Magharibi mwa Tanzania mpakani mwa Zambia na Tanzania. Eneo hili linajulikana kama Ufipa. Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alizaliwa Tarehe 05 Agosti 1944 katika familia ya mzee Joseph Pengo na Rozalia Nzyungu

Alibatizwa tarehe 06 Agosti 1944 na Padre Mmisionari wa Afrika (White Father)  Pd Joseph Bertsch na ndie alimpa jina la Polycarp. Siku ya somo wa Mtakatifu Polycarp huadhimishwa tarehe 23 Februari.

Alianza shule ya awali akiwa na umri mdogo sana katika shule ya masista Wamisionari wa Afrika karibu sana na nyumba ya Polycarp. Paroko wake alimshauri kujiunga na seminari ndogo ya Karema baada ya kuona wito wake. 1956 alijiunga na Seminari ya Karema darasa la tano katika Jimbo Katoliki la Karema, ambalo ndio Jimbo la Mpanda kwa sasa. Masomo yalifundishwa kwa lugha ya Kilatini, Kiingereza kilifundishwa kama lugha ya ziada

Alifaulu Cambridge School Certificate examinations akajiunga na Seminari ya Kipalapala Mkoa wa Tabora 1965 kwa ajili ya masomo ya Falsafa

Alipata daraja ya Upadre Juni 20. 1971 na Askofu Karoli Msikila katika Kanisa Kuu la Jimbo la Sumbawanga. Baada ya hapo aliteuliwa kuwa katibu wa Askofu Msikila kazi ambayo alikwisha ianza tangua awe shemasi. Miaka miwili baadae alikwenda kwa masomo  nchini Roma Julai 1973, Uteuzi ulifanywa akiwa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Alisoma masomo ya Teolojia ya Maadili (Moral Theology) ambayo yalifundishwa Kiitaliano.. Pale Roma aliishi na Mapadre Wamisionari wa Afrika akisoma Chuo Kikuu cha Laterano Accademia Alphonsiana. Baadae alihamia Collegio Urbano De Propaganda Fide kusomea shahada ya uzamili (Licensciate) na kupata Shahada ya uzamivu ya Maadili (Doctrate in Moral Theology) Desemba 1976.

Januari 1977 alihitimu masomo na kurudi nyumbani. Aliteuliwa kufundisha Seminari ya Kipalapala akijiandaa kufungua seminari ya Segerea wakati huo ujenzi ukiendelea. Seminari ya Segerea ilifunguliwa Januari 1979. Padre Polycarp alikuwa mwalimu wa Teolojia na Maadili akiwa na timu ya mapadre wengine. Pd Pengo alianzisha miradi ya kujitegemeza kulima na kufuga.

Askofu

Akiwa Segerea, Nov 25, 1983 siku ya Ijumaa Baba Mt Yohane Paulo II alimtangaza Padre Pengo kuwa Askofu wa pili wa Nachingwea na mzalendo wa kwanza kuongoza Jimbo hilo. Misa ya kupewa daraja ya Uaskofu ilifanyika Roma sikukuu ya Epifania Tar 6 Jan 1984 na Baba Mt Yohane Paulo wa II. Alikuwa Mtanzania wa kwanza kupewa daraja ya uaskofu na Papa Yohane wa II.

Tarehe 17 Oktoba 1986 Jimbo la Nachingwea Liliondolewa rasmi kwenye orodha ya majimbo ya Tanzania na Kuzaliwa Jimbo la Tunduru- Masasi, Askofu Polycarp Pengo akatangazwa kuwa Askofu mpya wa Tunduru- Masasi

Tarehe 22 Januari 1990 Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II alimtangaza Askofu Polycarp Pengo Kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati huo Hayati Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa akiwa Askofu Jimbo Kuu la Dar es Salaam akikaribia kustaafu.Askofu Pengo alikabidhi Jimbo la Tunduru- Masasi kwa Padre aliyeteuliwa kusimamia Jimbo hilo  Aprili 1990 na kuanza safari ya kuja Dar es Salaam. Aliishi Baraza la Maaskofu lakini alipenda sana kwenda Pugu kwa sala binafsi na ndio maana hadi leo amekuwa na mapenzi na Pugu.

Akiwa safarini kuelekea Morogoro kutoa daraja la Upadre Baba Mt. Yohane Paulo II alimtangaza kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, na siku hiyo hiyo Mwadhama Laurian Rugambwa alistaafu rasmi akiwa na miaka themanini.

Tarehe 17 Jan 1998 Baba Mtakatifu alitangaza kwamba amemteua Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Polycarp Pengo kuwa Kardinali mwezi mmoja baada ya kifo cha  Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa Desemba 08.1997.

Tar 22 Feb.1998, Ibada ya Kupewa Ukadinali ilifanyika huko Roma, katika Ibada hiyo Maaskofu Ishirini na watatu akiwemo Askofu Polycarp Pengo walipewa ukardinali ambao ameutumikia mpaka kufikia Tar 15 Agosti 2019 alipo mkabidhi Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa`ichi  kushika nafasi ya Uaskofu Mkuu wa Jimbo.