Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
MRATIBU
Mratibu ndiye mtendaji wa shughuli za kila siku, ni mwajiri, Mratibu huthibitishwa na kiongozi husika wa hierakia mahalia na kufanyakazi kama Mratibu wa Halmashauri ya Walei. Katika ngazi ya Jimbo, uteuzi wa Mratibu sharti uthibitishwe na Askofu wa Jimbo. Hii ni kwa kadiri ya Katiba ya Halmashauri Walei (5.2.6.2, Uk 17).
Majukumu na wajibu ni kama ifuatavyo;
· Kufanya kazi za kiofisi za Halmashauri Walei katika ngazi husika
· Kuratibu shughuli za kila siku za Halmashauri Walei
· Kuwa kiungo cha utendaji kwa wajumbe wa Kamati Tendaji za Vyama/Mashirika na Jumuiya za Kitume.
· Kushirikiana kwa karibu na Mkuu wa Idara/Mkurugenzi wa Idara ya Utume wa Walei ngazi ya Jimbo na Taifa
· Kubuni na kupendekeza majukumu ya Idara ya Utume wa Walei pamoja na mambo mengine yatakayoelekezwa
25/12/2025