Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Kamati Ndogo ya Afya na Mazingira ina jukumu la kutoa elimu kwa waumini kuhusu afya na mazingira. Kamati hii inashirikiana na taasisi za afya na mashirika ya mazingira kutoa huduma za afya, na kuhakikisha kuwa mazingira ya kanisa na jamii yanatunzwa na kulindwa. Kamati hii inahamasisha usafi, lishe bora, na kupambana na magonjwa, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kuhusu magonjwa yanayoenezwa na mazingira duni. Pia, kamati hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa jamii ya Kanisa inashiriki katika shughuli za kulinda na kutunza mazingira.
Wajumbe wa kamati hii watateuliwa kulingana na elimu au majukumu yao katika fani ya Afya na Mazingira. Wajumbe watateuliwa kutoka katika Halmashauri ya Walei na pale inapobidi watateuliwa kutoka kwa Walei wengine wabatizwa kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Wafuatao ni wajumbe wa Kamati ndogo ya Afya na Mazingira
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa uongozi Heiirakia na Halmashauri ya Walei kuhusu masuala ya afya na mazingira kwa jumla.
- Kuratibu utoaji wa elimu ya afya na mazingira kwa Halmashauri ya Walei Jimbo.
- Kusimamia utoaji Huduma ya kwanza kwenye mikusanyiko yote ya kijimbo.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya afya na mazingira kwa Parokia zitakazohitaji ushauri.
- Kutekeleza majukumu mengine yanayohusu huduma za afya yatakayojitokeza na au kuelekezwa na Hairakia/Halmashauri ya Walei.
- Kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati kila baada ya miezi mitatu