Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Kamati Ndogo ya Ardhi na Ujenzi inaratibu na kusimamia matumizi ya ardhi na mali za kanisa. Kamati hii ina jukumu la kufuatilia na kusimamia miradi ya ujenzi, kama vile ujenzi wa makanisa, shule, nyumba za mapadre, na majengo mengine ya kijamii. Inajitahidi kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa kulingana na viwango bora vya ujenzi na kwa manufaa ya jamii. Kamati hii pia inahusika na upangaji wa matumizi ya ardhi, ili kuhakikisha kuwa rasilimali za kanisa zinatumika kwa ufanisi na manufaa kwa waumini.
Wajumbe wa kamati hii watateuliwa kulingana na elimu au majukumu yao katika fani ya ujenzi/ uhandisi (Uhandisi / fundi wa Ujenzi, umeme, barabara, maji, mabomba, Sound System, Quantity Surveyors, Interior Designers, Contractors nk.). Wajumbe huteuliwa kutoka katika Halmashauri ya Walei na pale inapobidi watateuliwa kutoka kwa Walei wengine wabatizwa kulingana na mahitaji ya wakati husika.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa uongozi hairakia kuhusu ununuzi wa ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa uongozi hairakia kuhusu masuala yote yanayohusu menejimenti ya ardhi inayomilikiwa na Jimbo na Halmashauri ya Walei na yale yanayohusu miradi ya ujenzi.
- Kushauri hairakia kuhusu uendelezaji wa ardhi wenye tija.
- Kuandaa Hadidu za Rejea na kushauri/ kuratibu michakato ya kuwateua wataalamu mbalimbali wa kutoa Huduma za ushauri elekezi wa menejimenti ya ardhi na uendelezaji miradi ya ujenzi.
- Kufuatilia upatikanaji wa vibali mbalimbali vinavyohitajika katika hatua mbalimbali za ujenzi wa miradi kutoka mamlaka husika.
- Kupitia na kuidhinisha michoro ya awali na ile ya kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi.
- KuandaaHadidu za Rejeanakuratibumchakato wa kuteuawakandarasi kwa ajili ya uendelezajiwa miradi yaujenzi.
- Kusimamia hatua mbalimbali za uendelezaji wa miradi ya ujenzi na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa hairakia/Halmashauriya Walei pale unapohitajika.
- Kutoa taarifa za utekelezaji wa uendelezaji miradi ya ujenzi kwa hairakia na Halmashauri ya Walei kila baada ya Miezi mitatu.
- Kutoa ushauri wa masuala yote ya ujenzi na ardhi kwa Parokia zitakazohitaji.
- Kufanya majukumu mengine ya kitaalamu yanayohusu masuala ya ardhi na ujenzi kama yatakavyojitokeza na/au kuelekezwa na Hairakia au Halmashauri ya Walei.