KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Kamati
Kamati Ndogo ya Sheria na Katiba
Utangulizi

Kamati Ndogo ya Sheria na Katiba inatoa msaada wa kisheria kwa viongozi wa Kanisa na waumini. Kamati hii inajihusisha na uandishi na utekelezaji wa sheria na kanuni zinazohusu shughuli za Kanisa. Inasimamia na kutoa tafsiri ya katiba ya Kanisa na kuhakikisha kuwa inafuatwa. Kamati hii pia inajihusisha na masuala ya sheria ya ndoa, mali, haki za binadamu, na masuala mengine ya kisheria ambayo yanahusu jamii ya Kanisa. Hii inahakikisha kuwa Kanisa linatoa huduma kwa mujibu wa sheria na linaendeshwa kwa uwazi na haki.

Wajumbe wa Kamati

Wajumbe wa kamati hii watateuliwa kulingana na elimu au majukumu yao katika fani ya sheria. Wajumbe watateuliwa kutoka katika Halmashauri ya Walei na pale inapobidi watateuliwa kutoka kwa Walei wengine wabatizwa kulingana namahitaji ya wakati husika.

Wafuatao ni wajumbe wa kamati ndogo ya Sheria

No record found ....
No record...
Majukumu ya Kamati
  • Kushauri Halmashauri ya Walei (J) kupitia Kamati Tendaji (J) kuhusu mambo yote yanayohusu sheria katika ngazi zote za Halmashauri ya Walei Katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
  • Kushauri Uongozi Hiarakia wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuhusu mambo yote ya kisheria wanapotakiwa kufanya hivyo na uongozi Hiarakia katika ngazi yoyote.
  • Kupanga na kuratibu utekelezaji wa shughuli zozote za kisheria katika Jimbo Kuu la Dar es salaam za kila mwaka na kukubaliwa na Halmashauri ya Walei na Uongozi Hiarakia.
  • Kutoa taarifa kwa Hierakia na Kamati Tendaji ya Jimbo pale ambapo itaonekana taasisi ya Kanisa inaelekea kwenda kinyume na sheria ambazo zinaweza kuligharimu kanisa.
  • Kutoa elimu juu ya mambo ya kisheria katika Jimbo ili waamini wamwabudu Mungu lakini pasipo kuvunja sheria za nchi.
  • Kutoa ripoti ya hali ya haki na sheria kwa ujumla ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam kila baada ya Miezi mitatu (robo Mwaka) na kuiwakilisha kwenye Halmashauri ya Walei na Uongozi Hiarakia kupitia Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei(J).
  • Kuwa tayari kutekeleza kazi yoyote ya kisheria kwa wakati wowote inapoletwa na Uongozi Hiarakia na Halmashauri ya Walei ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.