KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Kamati
Kamati Ndogo ya Uinjilishaji
Utangulizi

Kamati Ndogo ya Uinjilishaji inajihusisha na kueneza Neno la Mungu kupitia shughuli mbalimbali za kiroho, mikutano, na maadhimisho ya kidini. Kamati hii inahamasisha waumini kushiriki katika shughuli za uinjilishaji, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya Neno la Mungu, mikutano ya kikatoliki, na kutoa huduma kwa wale wanaohitaji msaada wa kiroho. Kamati hii pia inaratibu shughuli za kufanya uinjilishaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashuleni, majumbani, na mtaa kwa mtaa. Inahakikisha kuwa waumini wanashirikiana kwa pamoja katika kazi ya kueneza imani ya Kikristo kwa njia ya upendo na mshikamano.

Wajumbe wa Kamati

Wajumbe wa kamati hii watateuliwa kulingana na utendaji wao wa kazi na uzoefu walionao katika kutekeleza majukumu ya Kamati. Wajumbe watateuliwa kutoka katika Halmashauri ya Walei na pale inapobidi watateuliwa kutoka kwa Walei wengine wabatizwa kulingana na mahitaji ya wakati husika

No record found ....
No record...
Majukumu ya Kamati
  • Kuielewa kwa kina, kuiishi inavyopaswa, kuifundisha kwa bidii na kuieneza Imani Katoliki;
  • Kuwezesha ufundishaji Biblia Takatifu na Maandiko mengine kuhusu Kanisa;
  • Kuwezesha ufundishaji wa Sakramenti mbalimbali za Kanisa;
  • Kuwezesha na kusimamia Uekumene na mahusiano na dini nyingine;
  • Kuratibu mafundisho ya dini shuleni;
  • Kufundisha mada mbalimbali kwenye Parokia, hasa parokia zinazohitaji kwa karibu kuwezeshwa vikuza imani, na katika taasisi mbalimbali za kama itakavyoelekezwa na Kamati Tendaji Halmashauri ya Walei Jimbo na Hirakia;
  • Kutekeleza kazi na majukumu mengine yoyote kadiri itakavyoelekezwa na Uongozi husika.