Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
Kamati Ndogo ya Ulinzi na Usalama ina jukumu la kuhakikisha usalama katika maeneo yote ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Inashughulikia usalama wa waumini wakati wa ibada, mikusanyiko, na maadhimisho ya kidini. Kamati hii pia inaratibu usalama wa mali za kanisa, pamoja na kuandaa mikakati ya kukabiliana na hatari na dharura zinazoweza kutokea. Inashirikiana na vyombo vya usalama vya serikali na mashirika ya kijamii kuhakikisha kuwa hali ya usalama inakuwa bora katika jamii.
Wajumbe wa kamati hii watateuliwa kulingana na elimu au majukumu yao katika fani ya Ulinzi na Usalama. Wajumbe watateuliwa kutoka katika Halmashauri ya Walei na pale inapobidi watateuliwa kutoka kwa Walei wengine wabatizwa kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Wafuatao ni wajumbe wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama
- Kushauri Halmashauri ya Walei (J) kupitia Kamati Tendaji (J) kuhusu mambo yote yanayohusu ulinzi na usalama katika ngazi zote za Halmashauri ya Walei Katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
- Kushauri Uongozi Hiarakia wa Jimbo Kuu la Dar es salaam kuhusu mambo yote ya Ulinzi na usalama wanapotakiwa kufanya hivyo na uongozi Hiarakia katika ngazi yoyote.
- Kupanga na kuratibu utekelezaji wa shughuli za ulinzi na usalama za Jimbo Kuu la Dar es Salaam za kila mwaka na kukubaliwa na Halmashauri ya Walei na Uongozi Hiarakia.
- Kutoa elimu ihusuyo masuala ya Usalama katika Parokia zilizopo ndani ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
- Kutafiti na kufuatilia masuala yoyote yale yanayoonyesha kuwepo na viashiria vinavyo hatarisha mazingira ya kuabudia na kuwanyima waamini amani wakati wa kuabudu.
- Kutoa ripoti ya Hali na Ulinzi na Usalama ya Jimbo Kuu la Dar es salam kila baada ya Miezi mitatu (robo Mwaka) na kuiwakilisha kwenye Halmashauri ya Walei na Uongozi Hiarakia kupitia Kamati Tendaji ya Halmashauri ya Walei (J).
- Kuwa tayari kutekeleza kazi yoyote ya ulinzi na usalama kwa wakati wowote inapoletwa na Uongozi Hiarakia na Halmashauri ya Walei ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.