Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa`ichi alizaliwa Tar 30 Desemba1953 kwenye familia ya Hayati Mzee Peter Mkilema Sinare na Mama Mary Barnaba Kitutu wa Mulo Kilema Jimbo Katoliki la Moshi. alibatizwa tar 6 Januari 1954 na kupata komunyo ya kwanza pamoja na Kipaimara mwaka 1964. Alisoma elimu ya legho Kilema na sekondari katika St. Jones Seminary Jimbo la Moshi, kisha katika seminari ya Kibosho mkoa wa Kilimanjaro. Alijiuga na elimu ya Teolojia katika seminari ya Kipalapala Jimboni Tabora. Alipokelewa rasmi kama Mkapuchini katika Seminari ya Kasita(Mahenge) Mwaka 1976 alifanya kiapo cha kwanza Januari 1977. aliprofesi mwaka 1981.
Alifanya uchungaji kuanzia Januari mpaka Mei 1980 katika Parokia ya Ruaha Jimbo la Mahenge na Juni mpaka Desemba 1980 nyumba ya upostulanti, Sofi, Jimbo la Mahenge.
Alipata ushemasi Julai 1981 Kasita Jimboni Mahenge na kisha daraja la upadre Tarehe 25 Nov 1981 katika Seminari ndogo ya Maua Jimbo la Moshi.
Mhs. Jude Thaddeus Ruwa`ichi alianza utume akiwa kama vicari wa Kasita Friary mwaka 1982 mpaka 1984 na pia akiwa Msaidizi wa Mkuu wa Unovisi . aliiunga kwa masomo zaidi ya uzamili wa falsafa kuanzia oktoba 1984 mpaka Juni 1986 katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoriana na baadae uzamifu katika falsafa kuanzia Oktoba 1986 mpaka Februari 1989.
Aprili 1989 mpaka Septemba 1989 alihudumu kama Paroko wa Mchombe Jimbo la Mahenge.
Kuanzia mwaka 1990 mpaka 1994 na kama Mshauri wa provinsi wa Wakapuchini. Na kwa upande Pronvinsi ya Tanzania katika kipindi tofauti alihudumu kama Mlezi na Mwalimu nchini Zambia --Maka 1989 mpaka 1991.
Alikuwa nyumba ya Fransiskani kwaajili ya masomo katika mji wa livingstone na baadae kuanzia 1991 mpaka 1994 katika chuo cha Mtakatifu Bonaventura.
Mnamo mwaka 1994 alichaguliwa kuwa Mjumbe wa nyumba Mama ya Wakapuchini, Mjini Roma- Italia ( Member of Capuchini General Definitory). alihudumu mpaka mwaka 1999.
Mwaka huo 1999 alitajwa kuwa Askofu mteule wa Jimbo Katoliki la Mbulu, na Tarehe16 Mei, 1999 alisimikwa rasmi kama askofu wa Jimbo hilo.
Kwa upande wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC);Mwaka 2000 mpaka 2003 alihudumu kama Mwenyekiti wa Tume ya Teolojia mwaka 2003 mpaka 2006. Alikuwa Mwenyekiti wa Idara ya Elimu na mwaka na 2006 mpaka 2012 akiwa kama Raisi wa Baraza la Maaskofu Tanzania. Na mwaka 2003 mpaka 2005 alikuwa mwenyekiti wa Baraza la SAUT (Chuo cha SAUT) na baadaye mwaka 2006 mpaka 2012 akiwa kama Kansela.
Mnamo 15 Januari 2005 aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo katoliki la Dodoma na kisha Tar 20 Februari 2005 alisimikwa rasmi kama askofu wa jimbo hilo.
Tar 10 Novemba, 2010 alipata uhamisho wa kwenda Jimbo Kuu la Mwanza na kusimikwa rasmi kama Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Tar 09, Januari 2011.
Alihudumu kama Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Shinyanga kwa kipindi cha kuanzia 07 Novemba, 2012 mpaka 02 Februari, 2015.
Tar 21 Juni, 2018 aliteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo kuu la Dar es salaam na kusimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu, wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Tarehe 15 Agosti, 2019.
Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam
Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafia dini iliyoambatana na Uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Askofu Mkuu alitangaza...
Ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala (Theotokos)
Katika adhimisho la misa Gezaulole eneo la Kigamboni, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi , miongoni mwao...
Neno la Askofu Mkuu kwa Halmashauri Walei
Natoa shukrani kwa Mungu kwa kuwepo na kustawi kwa Utume wa Halmashauri ya Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Utume ambao umenawiri hatua kwa hatua...
Majukumu ya Askofu wa Jimbo ni mengi, yanahusisha uongozi shughuli za kichungaji na kiutawala. Hapa chini ni baadhi tu ya majukumu ya Askofu Mkuu wa Jimbo
1. Kiongozi wa Kiroho
- Askofu ndiye Mchungaji Mkuu katika Jimbo.
- Huwaongoza watu wa Mungu, kuwapa mafundisho ya Imani na Maadili kulingana na mafundisho ya Kanisa Katoliki
2. Maadhimisho.
- Askofu hutoa Sakramenti hasa ile ya Kipaimara (Confirmation).
- Huongoza misa muhimu- kutoa Daraja Takatifu (kwa Mapadre na Mashemasi), na kusimamia ibada za kipekee kama vile kuwekwa wakfu kwa Makanisa au Madhabahu.
3. Askofu ni msimamizi wa Maklero wote ndani ya Jimbo lake.
- Anahakikisha wanatimiza majukumu yao ya kichungaji kwa uaminifu na uadilifu.
- Anayo mamlaka ya kuhamisha, kuteua, au kutoa vibali kwa mapadre kufanya kazi ndani ya Jimbo
4. Utawala wa Jimbo
- Anahakikisha Jimbo linaendeshwa vizuri kwa upande wa kiutawala, kifedha, na miundombinu.
- Husimamia taasisi zote za Kanisa katika Jimbo lake, kama vile shule, hospitali, mashirika ya misaada na taasisi za elimu ya juu za Kanisa. pia husikiliza changamoto mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi
5. Mshiriki wa Maamuzi ya Kanisa la Ulimwengu
- Askofu anaweza kuitwa kushiriki katika sinodi au baraza la Maaskofu katika ngazi ya kitaifa au kimataifa.
- Hushirikiana na Papa kupitia utii na mshikamano wa kichungaji.
16/02/2026
16/02/2026
21/11/2025
14/11/2025
14/11/2025
14/11/2025
Kanisa kuu Mbadala (Theotokos)
14/11/2025
14/11/2025
Kamati Tendaji H/Walei Jimbo Dsm
Kamati Tendaji H/Walei Jimbo Dsm
14/11/2025
14/11/2025
Pope audience
02/09/2023