KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Uongozi
Utawala & Utendaji

   "Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu 

Mhashamu . Vincent Lawrence Mpwaji
Askofu Msaidizi
Jimbo Kuu la Dar es Salaam

05 September 2026 - Current
Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo (Waefeso 1:3)

Mawasiliano

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Jumamosi tarehe 11 Julai 2026, na Vatican News, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Padre Vincent Lawrence Mpwaji kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Vatican News imeeleza wasifu wake kwa muhtasari kama ifuatavyo:

  • Alizaliwa tarehe 5 Juni 1978 mjini Morogoro, Tanzania.
  • Alisoma Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Anthony wa Padua, Ntungamo (Jimbo Katoliki la Bukoba).
  • Aliendelea na masomo ya Teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
  • Baada ya masomo yake ya Kikasisi tarehe 7 Julai 2008 alipewa Daraja takatifu ya Upadre.

Kwa upande wa utume wake wa kipadri, Vatican News imebainisha kuwa amewahi kuhudumu kama:

  • Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
  • Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
  • Wakili wa Mahakama ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam (2008–2011).
  • Mjumbe wa Kamati ya Miradi ya Jimbo Kuu.
  • Baadaye alitumwa na Jimbo kuu la Dar es Salaam kwa masomo ya juu Chuo Kikuu cha Kipapa katika Pontifical Gregorian University, ambako alipata Shahada ya Uzamivu mwaka 2021.
  • Tangu mwaka 2021 hadi uteuzi wake, amekuwa Chansela wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam.

Utume wa Uaskofu.

Tarehe 05 September 2026 ndiyo siku ambayo Padre Vincent Mpwaji aliwekwa Wakfu na kuwa rasmi Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam. Tukio hilo la kusimikwa kwake niliongozwa na Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwaichi, Askofu Mkuu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kuhushuriwa na Maashofu kutoka majimbo mbalimbali ya Tanzania pamoja na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Deogratias Ndejembi kama mgeni rasmi

 

Askofu Msaidizi (Auxiliary Bishop) Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Jimbo. Ana Daraja kamili la Uaskofu, lakini mamlaka ya mwisho ya kuongoza Jimbo ni ya Askofu Mkuu wa Jimbo au kwa mujibu wa sheria za Kanisa.

Baadhi ya majukumu yake ni:

  1. Kumsaidia askofu wa Jimbo katika kazi za kichungaji zikiwemo mipango ya Kichungaji ya Jimbo)
  2. Hutoa sakramenti (Kipaimara (Confirmation). Huadhimisha misa na Ibada mbalimbali za jimbo na pia huweka wakfu Mashemasi na Mapadre
  3. Humwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo kwenye matukio mbalimbali na kushughulikia sekta alizokabidhiwa. 
  4. Mshiriki katika uongozi na maamuzi mbalimbali kuhusu Jimbo
  5. Majukumu ya kisheria na kiutawala Vicar General au Episcopal Vicar, 
Similar Profiles