Dar es Salaam
Usaidizi wa Wateja
"Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu
Alizaliwa tarehe tarehe 8/1/1965 huko Moshi Kilimanjaro kwa wazazi Michael Ndetaramo Kyara na Aloisia Shewiyo Minja.
Alipata Elimu ya Msingi katika shule ya Lego Wilaya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kuanzia mwaka 1972 hadi mwaka 1979, akapata elimu ya Sekondari katika Seminari ya Mtakatifu Yakobo iliyoko Moshi kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1986. Alipata elimu ya falsafa katika Seminari Kuu ya Ntungamo Jimbo la Bukoba kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 1988. Pia akasomea Teolojia katika Seminari Kuu ya Kipalapala kwanzia mwaka1988 hadi mwaka 1994.
Tarehe 6 Januari 1994 alipewa daraja takatifu ya Ushemasi. Tarehe 24 Juni 1994 alipata daraja ya Upadri katika Parokia ya Mtakatifu Maximillian Kolbe - Mwenge. Baada ya kupata upadri aliteuliwa kuwa Katibu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam na Mkurugenzi wa Miito ambapo alifanya kazi kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 1998. Kisha aliteuliwa kuwa mkufunzi na mlezi wa Seminari Kuu ya Segerea kwa muda wa mwaka mmoja tu. Mwaka 1999 hadi 2012 alitumwa kwenda kusomea masomo ya Sheria za kanani (Canon Law) katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA) Kenya.
Baada ya masomo hayo aliteuliwa kuwa Mkufunzi wa Sheria za Kanoni katika Seminari Kuu ya Segerea na mwamuzi katika Mahakama ya Kanisa kuanzia mwaka 2001 hadi mwaka 2006. Baada ya hapo alitumwa tena kwenda kusomea Shahada ya juu ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Katoliki kilichopo Linz Austria kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2011. Baada ya kumaliza kusoma akarudi katika kazi ya ukufunzi wa Sheria za Kanisa katika Seminari Kuu ya Segerea na Mwamuzi wa Mahakama ya Kanisa, kuanzia mwaka huo 2011.
Tarehe 7 Julai 2021 aliteliwa na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Askofu wa heshima wa Jimbo
Askofu Msaidizi ni msaidizi wa Askofu mkuu katika shughuli za kichungaji
Askofu Msaidizi (Auxiliary Bishop) Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Jimbo. Ana Daraja kamili la Uaskofu, lakini mamlaka ya mwisho ya kuongoza Jimbo ni ya Askofu Mkuu wa Jimbo au kwa mujibu wa sheria za Kanisa.
Baadhi ya majukumu yake ni:
- Kumsaidia askofu wa Jimbo katika kazi za kichungaji zikiwemo; (Kutembelea Parokia na pia Mshiriki katika mipango ya Kichungaji ya Jimbo)
- Husimamia utoaji wa sakramenti (Kipaimara (Confirmation). Huadhimisha misa na Ibada mbalimbali za jimbo na pia huweka wakfu Mashemasi na Mapadre
- Humwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo kwenye Mikutano, Sherehe na kushughulikia sekta alizokabidhiwa na pia mshiriki wa maamuzi ya jimbo
- Kusaidia katika uongozi wa Jimbo
- Majukumu ya kisheria na kiutawala Vicar General au Episcopal Vicar,
27/05/2026
27/05/2026
27/05/2026
14/11/2025
14/11/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
01/09/2025
Uzinduzi wa Warsha ya Waamini
01/09/2025