KUHUSU HALMASHAURI YA WALEI
Uongozi
Utawala & Utendaji

   "Jubilei ya miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam - Tufanywe upya na Roho Mtakatifu 

Fredrick Wambura
Meneja Fedha Miradi ya Jimbo
Jimbo Kuu la Dar es Salaam

*     Mwamini Mlei

*     Muumini katika Parokia ya Mtakatifu  Vincent wa Paulo - Kibamba. Dekania ya Kibaha

*     Afisa Fedha Miradi ya Jimbo, Dar es Salaam 

*     Mjumbe wa Kamati ya Mavuno, Jimbo Kuu la Dar es Salaam

Afisa Fedha, Miradi Jimbo

  • Anahusika kupanga, kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha za miradi mbalimbali ya Jimbo. 
  • Kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi na kwa kufuata miongozo ya kifedha ya Jimbo na hata kanuni kadiri ya sheria za nchi.
  • Kuhakikisha uwepo wa mfumo thabiti wa uhasibu- kuratibu malipo, kuthibitisha stakabadhi, na kusimamia matumizi kwa kushirikiana na Ofisi ya Fedha kwa kuzingatia sera na kwa utaratibu wa Fedha.
  • Kuhakikisha usalama wa fedha, mali zisizohamishika, na kuweka kumbukumbu za fedha, malipo, bima, n.k.
  • Anahitaji kutoa ripoti za kifedha kwa uongozi wa Jimbo (Askofu, na Kamati ya Fedha) ili kuonyesha maendeleo ya miradi na uwazi wa matumizi.
  • Kuhakikisha matumizi ya fedha katika miradi yanazingatia kanuni za manunuzi, taratibu za kisheria, viwango vya taaluma na uwazi. 
  • Afisa Fedha anashirikiana na Kamati ya Fedha ya Jimbo kutoa ushauri kwa Askofu juu ya masuala ya kifedha na miradi.
  • Anafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Fedha, Mhasibu, na Kamati ya Fedha katika Jimbo ili kupatanisha malengo ya kimaadili ya kifedha.

 

Similar Profiles